Vijana wawili wa ki-Saudi walikamatwa katika mji mkuu wa Riyadh na Kamati ya Kukuza Maadili na Kuzuia Maovu (CPVPV) kwa madai ya kukashifu dini. Bader Al-Rasheed @BAlrasheed na Abdullah Al-Bilasi @3bdlla walisimulia yaliyowapata kwenye mtandao wa twita.
Kwa mujibu wa Al-Rasheed, walikuwa wamekaa nje ya mkahawa wakati gari la CPVPV lilipokuwa likipita kwa kuwaamuru watu kuondoka eneo hilo waende kwenye swala ya jioni. Alisema yeye alibishana na mtumishi mmoja wa CPVPV kama kuketi katika maeneo ya umma wakati wa saa za swala ilikuwa kosa.
Al-Rasheed baadaye alitwiti [ar]:
@BAlrasheed: لأني أول مرة أسمع بهذا النظام ولعلمي بأن الهيئة ومعظم الأجهزة الأمنية أحياناً يتصرفون حسب مزاجهم ويختلقون لك قوانين غير موجودة
رحت للجمس وسألت: هل هناك قانون يمنع الجلوس في الأماكن العامة وقت الصلاة؟
“@BAlrasheed: Kwa sababu ilikuwa ni mara ya kwanza mimi kusikia sheria hii na ‘heya'(neno la mtaani wanalooitwa CPVPV) mambo holela wakati mwingine, nilikwenda katika gari lao na kuuliza: kuna sheria inayopiga marufuku kukaa katika maeneo ya umma wakati sala?”
Jibu la mwajiriwa huyo lilikuwa kwamba ni haramu (imezuiliwa kidini), lakini Al-Rasheed aliingilia kati akisema:
@BAlrasheed: قاطعته وقلت: لا تقول لي يقول الرسول صلى الله عليه وسلم، فيه قانون؟ الحديث نصيحة وأنا حر أعمل بها أو لا و(لا إكراه في الدين) أما القانون فهو عقد اجتماعي بين المواطن والحكومة وهذا الشي اللي أنا ملزم به فقط.
“@BAlrasheed: Usiniambie dini inavyosema, je kuna sheria? Dini ni suala la uamuzi binafsi. Ni sheria tu ndiyo ninalazimika kutii.”
Kwa mujibu wa Al-Rasheed, mtumishi huyo alikasirika na akadai kitambulisho chake na cha rafiki aliyekuwa naye.
Kisha, mtumishi huyo wa CPVPV alianza kuwatishia na kuchochea maafisa wa polisi kuchukua hatua dhidi yao. Dakika chache baadaye, gari lingine la CPVPV na gari la polisi lilikuja kuwakamata na kuwapeleka katika kituo cha polisi cha al-Sulaimaniyah.
Al-Bilasi alisimulia kuhusu hali ya mbaya na unyama katika selo:.. “. Ilikuwa ndogo na yenye msongamano mkubwa. Hakukuwa na vitanda vyovyote au magodoro,” alisema “Tulilala sakafuni. Nilimwomba afisa magareza kuniruhusu nilale koridoni lakini yeye alinitukana tu, ” anaongezea.
Asubuhi iliyofuata, walichukuliwa, wakiwa wamepigwa pingu mkononi, kupelekwa kwa Ofisi ya Upelelezi na Mashtaka. Baada ya kuwasili hapo, walipelekwa kwa chumba kidogo ambapo walisubiri kwa masaa kadhaa kabla ya wao kuitwa kivyao kwa ajili ya mahojiano. Mpelelezi alimwambia Abdullah kwamba mtumishi wa CPVPV na maafisa wa polisi “si watu wa kubishana nao bali kuwatii.”
Jinamizi lao lilifikia mwisho wakati walipoachiliwa baada ya wazazi wao kuwawekea dhamana ingawa mpelelezi aliliita tukio hilo kuwa ni “kutokuelewana.” Polisi wa kidini hawakuridhishwa na kudai kwamba watu hao wawili washitakiwe.
Kichekesho zaidi, al-Bilasi na al-Rasheed waliripoti simulizi la mwaka kuhusu raia wa Lebanon waliyemkuta katika kituo cha polisi cha al-Sulaimaniyah ambaye alikamatwa kwa “tabasamu lisiloruhusiwa kidini”!
من أظرف القصص في التوقيف.. لبناني يعمل في السواني في الفيصلية محكوم عليه بخمس أيام. التهمة: “ابتسامة غير شرعية”
@balrasheed: Moja ya mambo ya ajabu zaidi kukutana nayo selo ilikuwa ni mfanyabiashara wa Lebanon ambaye alihukumiwa kifungo cha siku tano. Kosa lake: “Tabasamu lisiloruhusiwa na Sharia.”
Tukio hilo lilitokea tarehe 25 Machi, 2013.