- Global Voices in Swahili - https://sw.globalvoices.org -

Ukatili wa Polisi Nchini Macedonia: Miaka Miwili Baadae

Mada za Habari: Ulaya Mashariki na Kati, Macedonia, Haki za Binadamu, Harakati za Mtandaoni, Maandamano, Sheria, Siasa, Uandishi wa Habari za Kiraia, Uhuru wa Kujieleza, Utawala

Stop Police Brutality June 6 2013

Siku ya Alhamisi, Juni 6, katika kituo cha Skopje, Vuguvugu la Kupinga Ukatili wa Polisi litatimiza miaka miwili baada ya mauaji ya Martin Neshkovski, ambayo yalisababisha maandamano makubwa katika ngazi za chini kabisa [1] nchini Macedonia katika majira ya joto ya 2011. Tukio la Facebook [2][mk] kuhusu ibada ya kumbukumbu linaeleza:

Siku ya Alhamisi, Juni 6, saa 11 asubuhi, tutatembelea eneo la ulipofanyikia uhalifu huo na kuwasha mshumaa wa ishara ya kutukumbusha tulivyopoteza maisha machanga ya kijana wetu. Na akumbukwe!

Wakati wa kusanyiko hilo Vuguvugu la “Kuzuia ukatili wa polisi” litafanya mkutano na waandishi kuwasilisha ratiba ya shughuli za maadhimisho yake ya pili. Kwa kuongeza, tutawaunga mkono kwa wa-Turuki ambao wametoa upinzani kwa kumwaga damu zao wakipinga ukatili wa polisi siku za hivi karibuni […]