- Global Voices in Swahili - https://sw.globalvoices.org -

‘Sauti za Iran’ Mradi Unaowapa Sauti Raia Waishio Vijijini

Mada za Habari: Mashariki ya Kati na Afrika Kaskazini, Iran, Harakati za Mtandaoni, Uandishi wa Habari za Kiraia

Sauti za Iran [1] ni mradi ulioundwa kwa kutumia mafanikio ya mradi wa Ushahidi [2].  Sauti za Iran inakusudia kuripoti habari kuhusu miji midogo na vijiji vya Iran na vile vile kukusanya maombi na matatizo ya wananchi na kuyatuma kwa serikali na wabunge.