- Global Voices in Swahili - https://sw.globalvoices.org -

Rais Obama Kuitembelea Tanzania

Mada za Habari: Marekani, Tanzania, Mahusiano ya Kimataifa, Uandishi wa Habari za Kiraia

Rais wa kwanza wa Marekani mwenye asili ya Afrika, Barack Obama [1]anatarajiwa kuwasili jijini Dar es Salaam kesho alasiri kwa ziara ya kiserikali. Blogu ya Swahili Time imeweka ratiba ya ziara hiyo ya siku mbili [2]. Issa Michuzi aliweka video [3] inayomwonesha Rais Kikwete [4] wa Tanzania akizungumzia ziara hiyo.