- Global Voices in Swahili - https://sw.globalvoices.org -

Misri Inavyopoteza Miji ya Kihistoria

Mada za Habari: Mashariki ya Kati na Afrika Kaskazini, Misri, Harakati za Mtandaoni, Maandamano, Siasa, Uandishi wa Habari za Kiraia
Cairo..The city of a thousand pillars? Photograph from CairoObserver Facebook page. The red lines show buildings which obscure the minerates of mosques which is a signature of the Cairo horizon being lost to new development [1]

Cairo..Jiji la nguzo elfu? Picha kutoka kwenye ukurasa wa Facebook wa CairoObserver. Mistari myekundu ikionyesha majengo ambayo huziba minara ya misikiti ambayo ni alama muhimu ya jiji la Cairo inayopotea kwa ujenzi mpya unaondelea.

Cairoobserver atoa wito [2][ar] kwa wakaazi wa Misri kupitia mtandao wa Facebook [3] na Twita [4][ar] kufanya maandamano mbele ya majengo ya serikali, yanayohusika na mipango miji, kote nchini Misri kudai kusitishwa kwa kuharibiwa na kupotezwa kwa sura halisi ya kihistoria katika miji.

Jiji lenye minara elfu sasa ni jiji lenye nguzo elfu! Mji wa kihistoria ambao uliorodheshwa kama urithi wa dunia [5] katika miaka ya 70 sasa unakabiliwa na uharibifu na kubadilika kila sifa yake na viongozi wanaishughulikia hali hii kama jiji lisilo rasmi lisilodhibitika tena
[…]

Jiunge nasi Jumatano Juni 19, 2013, saa 05:00 ( Masaa ya Cairo) katika Maandamano mbele ya ofisi la Gavana wa Cairo [6]