- Global Voices in Swahili - https://sw.globalvoices.org -

Matatizo Makuu ya Raia wa Benin ni Yapi?

Mada za Habari: Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara, Benin, Maendeleo, Uandishi wa Habari za Kiraia, Uchumi na Biashara, Utawala

Tite Yokossi anafunua matokeo ya kura ya maoni iliyoendeshwa na Mfuko wa Zinsou ambao uliwauliza wananchi wa Benin ni yapi ndiyo matatizo yao makuu leo [1][fr]. Tatizo la kwanza lililoorodheshwa lilikuwa uwezo mdogo wa kufanya manunuzi miongoni mwa watumishi wa umma. Mengineyo ni uwezekano wa kupata fursa ya elimu, huduma ya maji safi, huduma za afya na umeme, ulinzi wa raia na misaada kwa wakulima.