- Global Voices in Swahili - https://sw.globalvoices.org -

Gwaride la Kwanza la Mashoga Nchini Lesotho

Mada za Habari: Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara, Lesotho, Afya, Haki za Binadamu, Haki za Mashoga, Uandishi wa Habari za Kiraia

Leila Hall anablogu kuhusu gwaride la kwanza la mashoga kuwahi fanyika [1] nchini Lesotho:

Tukio hilo limeandaliwa na Kikundi cha Kutoa msaada cha MATRIX- Shirika lisilo la kiserikali la Lesotho- linatetea haki za watu kama wasagaji, mashoga, wenye hisia za mapenzi kwa jinsia zote mbili, Wanaogeuza jinsia nchini humo. Shirika hilo, ambalo lilitambuliwa kisheria mwaka 2010, kama lilivyo gwaride la mwaka huu ni shirika la kwanza la aina yake nchini Lesotho.