- Global Voices in Swahili - https://sw.globalvoices.org -

Uchaguzi Tume ya Uchaguzi Msumbiji: Mwanaharakati Ajitoa Kugombea

Mada za Habari: Msumbiji, Siasa, Uandishi wa Habari za Kiraia, Uchaguzi, Utawala

Kutokuwepo uwazi na weledi katika mchakato wa kumchagua mgombea, mbali na kufahamika nani hasa watachukua nafasi zinazogombewa kabla hata ya uchaguzi katika taasisi hiyo. Hizo zilikuwa baadhi ya sababu zilizotolewa na mwanaharakati wa haki za binadamu, Benilde Nhalivilo, wakati akijitoa rasmi kugombea nafasi kwenye Tume ya Taifa ya Uchaguzi ya Msumbiji [1][pt], chombo kinachohusika na kuandaa na kusimamia chaguzi nchini humo. Taarifa zaidi zinapatikana kwenye gazeti la A Verdade [2][pt].