- Global Voices in Swahili - https://sw.globalvoices.org -

Shambulio la Mabomu Mawili ya Kujitoa Muhanga Nchini Niger Yaua Watu 23

Mada za Habari: Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara, Mali, Naija, Dini, Habari za Hivi Punde, Mahusiano ya Kimataifa, Majanga, Uandishi wa Habari za Kiraia, Vita na Migogoro

Benjamin Roger wa Jeune Afrique anaripoti [1] [fr] kuwa wanajeshi 18, raia mmoja na magaidi wanne waliuawa mapema subuhi ya leo katika shambulio la mabomu ya kujitoa Muhanga kwenye gari mjini Agadez, Niger tarehe 23 Mei. Anaongeza kuwa wanafunzi wa chuo cha kijeshi wametekwa na gaidi mwingine kufuatia mabomu hayo. Wakati huo huo, gari jingine lilipuka kwenye mgodi wa madini ya Uraniam unaomilikiwana Kampuni ya Areva Group mjini Arlit, Niger. Kikundi cha kijeshi cha MOJWA [2] kimedai kuhusika na mashambulio hayo mawili.