- Global Voices in Swahili - https://sw.globalvoices.org -

Rafael Correa Aapishwa kwa Kipindi cha Tatu Kama Rais wa Ekuado

Mada za Habari: Uandishi wa Habari za Kiraia

Rafael Correa amekabidhiwa madaraka kuwa Rais wa Jamhuri ya Ekuado kwa kipindi kingine mpaka mwaka 2017.

Correa aliianza awamu yake ya tatu katika Bunge akishuhudiwa na wakuu wa nchi kadhaa za Marekani ya Kusini na Ulaya, wawakilishi wa kimataifa, wabunge, mawaziri, wanafamilia wake na wanachama wa chama tawala cha  Alianza PAIS [1]. Correa na Makamu wake Jorge Glas waliapishwa na Rais wa Bunge, Gabriela Rivadeneira, asubuhi ya Mei 24, 2013.

Katika hotuba yake ya kuapishwa Rais Rafael Correa aliahidi kuendelea na mipango ya kijamii ambayo ndiyo iliyochangia umaarufu wake mkubwa. Correa alisisitiza kuwa uwekezaji wa umma utaendelezwa mwaka huu kwa asilimia 15 ya Pato la Ndani (GDP) kuendelea na mipango ya kijamii na kujenga miundo mbinu.

Posesión de mando del presidente Rafael Correa. Quito, Ecuador, 24 mayo de 2013. Foto de  Presidencia de la República del Ecuador en Flickr. (CC BY-NC-SA 2.0) [2]

Rais Rafael Correa mara baada ya kukabidhiwa madaraka ya kuongoza nchi yake. Quito, Ecuador, Mei 24, 2013. Picha kutoka
Ofisi ya Rais wa Jamhuri ya Ekuado kwneye mtandao wa Flickr. (CC BY-NC-SA 2.0)

Katika mtandao wa twita wananchi wa Ekuando walitoa maoni yao kuhusiana na hotuba hiyo kwa kutuma alama habari #PosesiónPresidencial [3] [es] (Rais akabidhiwa madaraka).

Carlos Macas (@CarlosMacas19 [4]) [es] alitaja moja wapo ya mabadiliko ya Tume ya Pamoja Kimarekani kwa Haki za Binadamu (IACHR) [5] kwamba Correa alipendekeza [6] [es]: mabadiliko ya makao makuu kutoka Washngton kwenda kwenye nchi iliyopo kwenye bara hilo ambayo ilijiunga na Tume ya Pamoja ya Kimarekani kwa Haki za Binadamu [7] (inayofahamika pia kama Maridhiano ya San José).

@CarlosMacas19: [8] Rafael Correa “La sede de la CIDH tiene que estar en un País, que haya ratificado el pacto de San Jose” #PosesiónPresidencial [3] RT

@CarlosMacas19: [8] Rafael Correa “Makao Makuu ya Tume hiyo (IAHCR) ni lazima yawe katika nchi inayoridhia Makubaliano ya San Jose” #PosesiónPresidencial [3] RT

Lakini mwanasheria na mwanaharakati wa kisiasa Luis A. Gaibor G. (@Luisgaiborg [9]) [es] aliuliza:

@Luisgaiborg [10]: De q sirve q #Ecuador [11] firme todos los Pactos d D. Humanos si ni siquiera se respeta el Derecho d Libertad d Expresión #PosesionPresidencial [12]

@Luisgaiborg [10]: Inajalisha nini kama #Ecuador [11] itatia saini Makubaliano yote ya Haki za Binadamu kama haiheshimu Haki ya Uhuru wa Kujieleza #PosesionPresidencial [12]

President Correa ana mahusiano ya karibu sana [13] [es] na vyombo vya habari [14] nchini humo. Katika hotuba yake alisema “vyombo vya habari katika Bara la Amerika ya Kusini, ukiacha mifano michache kama ilivyo kawaida, ni vibovu, vibovu sana” na akadai kuwa mhanga wa “kufa kwa vyomvo vya habari”. Hata hivyo, kama mtaalamu wa mawasiliano ya umma Edison Pérez (@edyelrojo) [15] [es] alivyosema, Correa aliongeza: “Tutautetea uhuru wa kujieleza wa wananchi wote wa Ekuado na sio makundi fulani fulani pekee”.

Luis Baque Gutiérrez (@baquelig) [16] [es] alirudia maneno ya rais katika hotuba yake:

@baquelig [17]#PosesiónPresidencial [3] Este ECUADOR no esta dispuesto a ser colonia de nadie. Bravo @MashiRafael [18]

@baquelig [17]#PosesiónPresidencial [3] UKUADO haiko tayari kuwa koloni ya yeyote. Heko @MashiRafael [18]

Kwa mtazamo wa kina zaidi, @Jose_CastroS [19] [es] wa Guayaquil alihoji maneno ya Correa  alipotamka [20] [es] kwamba “Papa ni Mu-Ajentina, Mungu huenda ni Brazili (kama alivyowahi kusema Rais wa Brazili Dilma Rousseff), kwa hiyo ni hakika kuwa paradiso ni Ekuado”:

@Jose_CastroS [21]: que Ecuador es el paraiso ? donde deja la delincuencia, el narcotrafico , asesinatos? #PosesiónPresidencial [3]#CorreistaPendejo [22]

@Jose_CastroS [21]: Kwa hiyo Ekuado ni paradiso? Vipi vitendo vya jinai, usafirishaji wa madawa ya umma, mauaji? #PosesiónPresidencial [3]#CorreistaPendejo [22]

Mwisho, Elector Ecuador (@ElectorEcuador [23]) [es], mradi wa kiraia ambao unawahabarisha wapiga kura kuhusu wagombea wa uchaguzi [24] nchini humo, alimpongeza Correa na makamu wake:

@ElectorEcuador [23]: #Ecuador [11] Felicitamos en su nuevo mandato a @MashiRafael [18] y @JorgeGlas [25] #24deMayo [26] #EleccionesEC [27] http://fb.me/1X8pM9zO4 [28]

@ElectorEcuador [23]: #Ecuador [11] Tunampongeza @MashiRafael [18] na @JorgeGlas [25] kwa kushinda kipindi kingine cha uongozi #24deMayo [26] #EleccionesEC [27] http://fb.me/1X8pM9zO4 [28]