Mei, 2013

Habari kutoka Mei, 2013

Msumbiji: Madaktari Watangaza Mgomo

Madaktari nchini Msumbiji wametangaza rasmi kuwa wanaingia kwenye mgomo. Wanadhani “walikandamizwa, kutukanwa na kunyanyaswa” katika mkutano wao wa mwisho na serikali. Mgomo huu wa sasa unafuatia mgomo wa madaktari uliofanyika mapema mwaka huu. Tangazo kwa njia ya video linapatikana likiwa na tafsiri kwa maandishi ya kiingereza, na katika lugha kadhaa.

Mwanamke Aokolewa Kwenye Kifusi Baada ya Siku 17

  15 Mei 2013

Siku ifananayo na ile iliyogharimu maisha ya watu mara baada ya kuporomoka kwa jengo la ghorofa tisa huko Savar pembezoni mwa mji mkuu wa Banglasesh, Dhaka, idadi ya watu waliofariki imeongezeka hadi 1,055 , idadi inayopelekea tukio hili kuwa tukio lililowahi kuua watu wengi zaidi tokea lile la tarehe 9/11 kulipotokea mashambulizi ya kigaidi, mfanyakazi mwanamke ajulikanaye kwa jina la Reshma Begum amekutwa akiwa hai mara baada ya kuzuiwa na kifusi cha jengo hilo kwa siku 17.

Uchaguzi Tume ya Uchaguzi Msumbiji: Mwanaharakati Ajitoa Kugombea

  11 Mei 2013

Kutokuwepo uwazi na weledi katika mchakato wa kumchagua mgombea, mbali na kufahamika nani hasa watachukua nafasi zinazogombewa kabla hata ya uchaguzi katika taasisi hiyo. Hizo zilikuwa baadhi ya sababu zilizotolewa na mwanaharakati wa haki za binadamu, Benilde Nhalivilo, wakati akijitoa rasmi kugombea nafasi kwenye Tume ya Taifa ya Uchaguzi ya...

Pakistan: Imran Khan Aanguka na Kuumia Akiwa Kwenye Jukwaa la Kampeni

  11 Mei 2013

Aliyekuwa mchezaji maarufu wa kriketi na kisha kuamua kuwa mwanasiasa, ambaye kampeni yake ina tumaini kubwa la kuleta "Pakistan Mpya" aliyeweza kushawishi idadi kubwa ya vijana pamoja na wapiga kura wanaotokea mijini katika mikutano yake, alivunjika vifupa vitatu vya uti wa mgongo pamoja na mbavu baada ya kuanguka kutoka kwenye winchi iliyokuwa katika kimo cha futi 15 mda mfupi kabla ya kuhutubia. tukio hili limeonekana kuliunganisha tena taifa hili lililojigawa kwa visasi vinavyotokana na uchaguzi utakaofanyika mapema wiki hii.

Bangladesh: Waislamu Wadai Wanawake Wabaki Majumbani

  8 Mei 2013

Wanachama wa kikundi chenye msimamo mkali cha Kiislamu nchini kimewashambulia wanahabari wa kike waliokuwa wakitekeleza majukumu yao ya kiuandishi wakati kikundi hicho kilipokuwa kikifanya maandamano katika jiji la Dakar kudai kutumika kwa sheria kali za kiislamu, ikiwa ni pamoja na kupiga marufuku wanawake kuchanganyika na wanaume. Mpaka madai yao yatakapotekelezwa, chama hicho kimejiapiza kulitenga jiji la Dhaka na sehemu nyingine za nchi hiyo ifikapo Mei 5, 2013 kwa kuwaweka wanaharakati wake katika maeneo sita ya kuingilia jiji hilo.