- Global Voices in Swahili - https://sw.globalvoices.org -

Mwandishi Habari za Kiraia wa Miaka 14 Auawa Akiripoti Mapigano Nchini Syria

Mada za Habari: Mashariki ya Kati na Afrika Kaskazini, Syria, Habari za Hivi Punde, Haki za Binadamu, Uandishi wa Habari za Kiraia, Uhuru wa Kujieleza, Vita na Migogoro, Vyombo na Uandishi wa Habari

Omar Qatifaan, Mwanaharakati wa Habari mwenye umri wa miaka 14, aliuawa Mei 21, 2013 wakati alipokuwa anaripoti mapigano kati ya Jeshi la Syria na waasi wanaopinga serikali ya nchi hiyo kusini mwa al-Ballad eneo la Syria karibu na mpaka na Jordan.

Nyaraka kuhusu Syria [1] zilizotolewa na Mradi wa vyombo vya habari vya vijana ziliripoti kuhusu kifo chake, na  blogu ya habari  nchini humo YALLA SOURIYA [2] ilimwita kijana huyo kuwa “Roho wa Syria”.

Mgogoro wa Syria, kama vile Mapinduzi mengine yaliyozikumba nchi za Kiarabu, zimesababisha kuongezeka kwa waandishi wa habari za kiraia wanaoripoti kutoka katika kwenye uwanja wa vita kuhusu mgogoro unaoendelea kati ya majeshi yanayounga mkono serikali na yale ya waasi. Wengi wamekuwa kizuizini, kuteswa, na hata kuuawa wakiwa katika jitihada za kuutangazia ulimwengu habari za mapinduzi [3].

Watoto pia wameumia kupindukia wakati wa vita, na maelfu wakiuawa [4] wakati wa ghasia hadi wakati huu.

Media activist Omar was 14 year when he was killed while covering a battle in Daraa, Syria. Source: Twitter account of ‏@RevolutionSyria [5]

Mwanaharakati wa Vyombo vya Habari Omar Qatifan alikuwa na umri wa miaka 14 alipouawa akiwa anaripoti habari za vita huko Daraa, Syria. Picha kutoka akaunti ya twita ‏@RevolutionSyria [5]

Mwanaharakati mwingine wa  vyombo vya habari alirekodi video ya Qatifaan mara tu alipouawa. Video hiyo iliwekwa kwenye YouTube na SyrianDaysOfRage [6]: [NI VIDEO INAYOTISHA]: