- Global Voices in Swahili - https://sw.globalvoices.org -

Msumbiji: Madaktari Watangaza Mgomo

Mada za Habari: Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara, Msumbiji, Afya, Habari za Hivi Punde, Maandamano, Maendeleo, Uandishi wa Habari za Kiraia
Screenshot from press conference video [1]

Picha ya video ya mkutano na vyombo vya habari

Madaktari nchini Msumbiji wametangaza rasmi kuwa wanaingia kwenye mgomo. Wanadhani “walikandamizwa, kutukanwa na kunyanyaswa” katika mkutano wao wa mwisho na serikali. Mgomo huu wa sasa unafuatia mgomo wa madaktari uliofanyika mapema mwaka huu. Tangazo kwa njia ya video [1] linapatikana likiwa na tafsiri kwa maandishi ya kiingereza, na katika lugha kadhaa.