- Global Voices in Swahili - https://sw.globalvoices.org -

Michoro ya Dar: Sanaa kwa Maendeleo Endelevu

Mada za Habari: Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara, Tanzania, Sanaa na Utamaduni, Uandishi wa Habari za Kiraia

Dar Sketches [1] (Michoro ya Dar) ni sehemu ya mradi unaoanzia ngazi ya Mtaa jijini Dar Es Salaam, Tanzania ulioanzishwa na msanii na mchoraji Sarah Markes:

Ni katika kuenzi urithi wa kitamaduni na wa sanaa ya ubunifu wa majengo kwa jiji la Dar Es Salaam sambamba na juhudi za kukuza uelewa kwa wananchi juu ua tishio la urithi huu linalotokana na kasi kubwa ya kupanuka holela kwa jiji hilo.