- Global Voices in Swahili - https://sw.globalvoices.org -

Mfululizo wa Tamthilia ya Runinga ya Nchini Tanzania

Mada za Habari: Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara, Tanzania, Filamu, Sanaa na Utamaduni, Uandishi wa Habari za Kiraia

The Team Tanzania [1] (Timu Tanzania) ni mfululizo wa Tamthilia ya Runinga yenye kuzungumzia:

[…] Bi. Wito, mwalimu mahiri wa somo la uraia, anaigeuza kabisa mitazamo ya vijana makinda watatu anapowauliza maswali mazito mfano “Wewe ni nani”? vijana wale wenye umri wa miaka 16, waliofahamiana vyema tangu wakikua. Katika kuingia katika umri wa utu uzima, vijana hao wanatafuta kujitambua huku wakikabiliwa na misongo mingi ya kifamilia na kiutamaduni.