- Global Voices in Swahili - https://sw.globalvoices.org -

Kwa nini Mashirika ya Umma Yameshindwa Nchini Zambia

Mada za Habari: Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara, Zimbabwe, Siasa, Uandishi wa Habari za Kiraia, Uchumi na Biashara

Elias Munshya, mwanasheria na mchungaji wa Zambia, anaeleza [1] kwa nini mashirika ya umma yamedumaa nchini Zambia tangu uhuru:

Mashirika ya umma hayajawahi kutengeneza faida tangu mwaka 1964. Yamekuwa yakiendeshwa kiholela bila utaalamu wa kibiashara bali kisiasa. Mashirika haya hayajawahi kuwa na wataalamu wanaoendesha bodi husika bali yamejaa wafanyakazi kwa misingi ya mahusiano ya undugu, ubinamu, upwa na ujukuu na wanasiasa

.