6 Mei 2013

Habari kutoka 6 Mei 2013

TEDXSão Tomé: Mkutano Wanukia São Tomé na Príncipe

Uandikishaji wa awali kwa ajili ya mkutano wa TEDXSão Tomé umezinduliwa rasmi. Mkutano huo una kaulimbiu inayosema “Visiwa Vimeunganishwa : São Tomé + Príncipe = Áfrika Vimeunganishwa na Ulimwengu” na utafanyika tarehe 20 Juni. Wasemaji katika mkutano huo waliothibitishwa ni pamoja: Dynka Amorim, Ismael Sequeira, Profesa Robert Drewes na Aoaní...

China Yadhibiti Habari za Maandamano Yakupinga Kujenga Kiwanda cha Kemikali

  6 Mei 2013

Wakazi wa jiji la kusini magharibi mwa China liitwalo Kunming waliingia mtaani mnamo Mei 4, 2013 kupinga mpango wa kuzalisha kemikali zenye sumu karibu na makazi yao. Vyombo vya Habari vya serikali havikutangaza habari za maandamano hayo, na katika hali ya kushangaza wafuatiliaji wa mtandaoni wamefuta habari na picha zinazohusiana na maandamano hayo kwenye mtandao maarufu wa kijamii uitwao Sina Weibo tangu Mei 4, 2013.