- Global Voices in Swahili - https://sw.globalvoices.org -

Vyama vya Siasa Msumbiji na Matumizi ya Intaneti

Mada za Habari: Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara, Msumbiji, Siasa, Uandishi wa Habari za Kiraia, Uchaguzi

(…) kuna nafasi ambayo mpaka sasa haijatumiwa ipasavyo na vyama vya siasa nchini Msumbiji, iwe ni kwa ajili ya kueneza propaganda za kisiasa au kufanya kampeni za uchaguzi: nalo ni mtandao wa intaneti.

Jukwaa la Msumbiji liitwalo Olho Cidadão [1] (Jicho la Wananchi) lilizindua blogu mpya tarhe 2 Aprili, 2013, kwa uchambuzi wa uwepo wa vyama vya siasa mtandaoni [2] [pt]. Msumbiji itafanya uchaguzi wa manispaa tarehe 20 Novemba mwaka huu.