- Global Voices in Swahili - https://sw.globalvoices.org -

Serikali ya Bangladeshi Yawafuatilia Wanablogu, Yawatuhumu Kuukashfu Uislam.

Mada za Habari: Asia ya Kusini, Bangladesh, Dini, Haki za Binadamu, Harakati za Mtandaoni, Maandamano, Siasa, Uandishi wa Habari za Kiraia, Uhuru wa Kujieleza, Utawala

Makala hii ni sehemu ya makala zetu maalum za maandamano ya Bangladeshi Bangladesh's #Shahbag Protests [1]

Kadri vurugu kali kati ya wanaharakati wa Kiislamu na serikali [2] zinaendelea kuongezamvutano wa kidini [3] nchini Bangladeshi, mamlaka ya mawasiliano ya Bangladeshi inaweka juhudi za kuwanyamazisha wanablogu wakiwadhania kuwa wapo kinyume na Uislamu au kinyume na serikali.

Mwanablogu aliyewahi kutunukiwa tuzo, Asif Mohiuddin pamoja na wanablogu wengine watatu siku za hivi karibuni wamekuwa wakifuatiliwa na tume ya kudhibiti mawasiliano ya Bangladeshi, hii ni kwa mujibu wa tovuti ya habari za mtandaoni ya Timesworld24.com [4] [bn]. Siku za hivi karibuni, tume hii iliwasiliana na blog.net, ambao ni uwanja mpana kwa wanablogu nchini Bangladeshi, ikiutaka mtandao huu kuziondoa blogu hizi nne kutoka kwenye mtandao huo.

Kwenye taarifa iliyopo kwenye mtandao wao, Somewhereinblog.net [5] ilitangaza rasmi kuwa ilishaziondoa blogu hizo nne kama njia ya kutimiza agizo la serikali.

Serikali ya Bangladeshi iliunda [6] [bn] tume ya watu wanne mnamo tarehe 13 Machi 2013 ili kuwafuatilia wanablogu na watumiaji wa Facebook waliotoa kauli za kuukashfu uislam pamoja na Nabii Mohammad. Tume ya Udhibiti wa Mawasiliano nchini Bangladeshi imeomba taarifa za idadi fulani ya wanablogu kutoka katika sehemu mbalimbali zitumiwazo na wanablogu kuweka taarifa mbalimbali ikiwa ni juhudi za kutaka kuwanyamazisha waandishi fulani wanaosadikiwa kuukashfu Uislamu au kutaka kuiangusha serikali.

Hatua hii inakuja baada ya Waislamu kudai kuwa [7] wanablogu wanaosaidia harakati za Shahbag [1] zinazoendelea na zinazodai adhabu kubwa kwa wahalifu wa kivita nchini humo, ambao miongoni mwao ni viongozi wakubwa wa chama kikubwa cha Kiislam cha Jamaat-e-Islami [8] – ni wale wasiomwamini Mungu na wanaoshinikiza hali ya kutokuwepo kwa uchangamano.

Baadhi ya wanaharakati wa Kiislam wamefika mbali na kutangaza kuwa wanablogu wa Shahbag watachinjwa [9] hadharani. Mwanablogu Ahmed Rajib Haider [10], ambaye alikuwa mstari wa mbele kwenye harakati za Shahbag na pia ndiye aliyeandika mara kwa mara kuhusiana na uumini ukereketwa wa kidini nchini Bangladesh aliuawa kikatili [11] nje kidogo ya nyumbani kwake katika mji mkuu Dhaka mnamo Februari 15, 2013.

Mohiuddin, aliyejitangaza hadharani kuwa ni mtu asiyeamini Mungu, amekuwa akizungumzia harakati za Shahbag na aliandika kupinga dini na siasa za udini. Lakini kama kweli kublogu kwake kunachangia lolote katika vurugu za kidini na chuki bado haujadhibitishwa. Januari 2013, alishambuliwa kikatili [12] na washambuliaji ambao hawakujulikana, pengine kutokana na maandiko yake. Siku za hivi karibuni, polisi waliwatia nguvuni watu wanne [13] waliojitokeza na kusema kuwa ndio waliomshambulia Mohiuddin kufuatia maelekezo ya watu wenye msimamo mkali wa kidini.

Kwanye mahojiano na Deutsche Welle Syeda Gulshan Ferdous Jana [14], muasisi wa Somewhereinblog.net alisema:

hii ni mara ya kwanza katika kipindi cha miaka saba cha somewhereinblog.net kwa serikali kutoa maelekezo ya maandishi ili kuadabisha wanablogu. Barua pepe hiyo iliwataja wanablogu wane ikiwemo taarifa ya blogu kumuhusu Asif Mohiuddin, na kutushauri kuziondoa moja kwa moja blogu hizi haraka iwezekanavyo.

Mohiuddin, ambaye blogu yake [15] ilishinda tuzo ya blogu bora ya uanaharakati wa kijamii [16] kutoka kwenye Tuzo ya Blogu bora ya Deutsche Welle, 2012, amepata upinzani mkubwa sana kufuatia maandiko aliyokwisha kuyaandika. Aliwekwa kizuizini mwaka 2011 wakati wa maandamano ya mitaani na polisi walipendekeza [17] kuwa ingekuwa vyema angeacha kuandika.

Blogger Asif Mohiuddin. Image by Siam Sarower Jamil. Copyright Demotix (10/2/2013) [18]

Mwanablogu Asif Mohiuddin. Picha na Siam Sarower Jamil. Haki miliki Demotix (10/2/2013)

Mnamo Machi 20, 2013, Mohiuddin na wanablogu wengine saba walifunguliwa mashtaka na mtu mmoja huko katika wilaya ya Natore, Kaskazini mwa Bangladesh [19] [bn] kwa makosa ya kutoa taarifa za uongo kuhusu uislam, Mungu na Nabii Mohammad. Kesi nyingine dhidi ya wanablogu hawa ilitupiliwa mbali mnamo tarehe 6, Machi 2013 kufuatia kukosekana kwa ushahidi.

Mohiuddin alitoa maoni yake kwenye ukurasa wa Facebook [20] [bn] kuhusiana na hali ya hivi karibuni ya kuzuiwa kwake:

প্রায় প্রতিদিন ধর্মের পক্ষে অসংখ্য ব্লগে অসংখ্য লেখা পোস্ট হয়। অথচ অনলাইনে শুধুমাত্র “আমি প্রচলিত ধর্মে অবিশ্বাসী” এই কথাটুকু বলার অপরাধে অসংখ্য অশ্রাব্য গালিগালাজের সম্মুখীন হয়েছি।

Kila siku, makala nyingi zinazopakiwa zinazungumzia dini. Lakini nilipoandika tu kuwa, “siamini katika dinni za jadi”, nilishambuliwa na wengi.

Katika makala hiyo, alizichukulia juhudi za tume iliyoundwa za kuzinyamazisha blogu kuwa ni jambo hatari linaloweza kutumiwa wakati mwengine kwa matukio yanayofanana na haya. In the same post, he called the commission's efforts to shut down blogs a dangerous precedent:

কোন ব্লগারের লেখা সেই ব্লগটির নিজস্ব আইন অনুসারে বেআইনী মনে হলে বা শর্তাবলী লঙ্ঘিত হয়েছে বলে মনে হলে ব্লগ কর্তৃপক্ষই তার সিদ্ধান্ত নেবে। ব্লগ কর্তৃপক্ষ এই বিষয়ে স্বাধীন এবং কোন লেখা থাকবে আর কোন লেখাটি থাকবে না, তা সিদ্ধান্ত নেয়ার দায়িত্ব কোনভাবেই কোন ক্ষমতাশালী মহলকে দেয়া যাবে না। ভেবে দেখুন, আজ এই অজুহাতে কারো ব্লগ সরকার বন্ধ করে দিতে সক্ষম হলে সরকার ভেবে নেবে ব্লগারদের তারা নিয়ন্ত্রণ করতে সক্ষম। তাই কাল আরেকজন ব্লগারের ব্লগও তারা বাতিল করার আবদার তুলবে। কোন সরকারই অনন্তকাল থাকবে না, আগামিতে কোন ধর্মান্ধ গোষ্ঠী ক্ষমতায় চলে আসলে পরিস্থিতি কোনদিকে যাবে?

Kama maandiko ya mwanablogu yeyote hayatii kanuni yoyote ya blogu husika, au kuaminika kuwa siyo rasmi, bila shaka mmiliki wa blogu anaweza kuamua lolote kuhusiana na hili. Makala zipi zichapishwe na zipi zisichapishwe, inapaswa kuwa kwa maelekezo ya jukwaa la blogu na si mamlaka za udhibiti. Hebu fikiria, kama mamlaka zinaweza kuzinyamazisha sauti kwa kuyalazimisha majukwaa kufanya hivyo, wanaweza kuanza kuamini kuwa wanaweza kuwaongoza wanablogu nini cha kufanya. Kwa hiyo watatafuta sababu nyingine ya kuifungia blogu nyingine. Serikali itabadilika na kudhani iwapo serikali yoyote yenye msimamo mkali wa Kiislam ikiingia madarakani ni kitu gani kitatokea?

Katika mahojiano na radio Deutsche Welle Mohiuddin [21] alisema kuwa hatakata tamaa kublogu.

Stop authoritarian aggression against bloggers. Blogging is our right. Image courtesy Asif Mohiuddin [22]

“Sitisha vitisho vya nguvu dhidi ya wanablogu. Kuandika kupita blogu ni haki yetu.” Picha kwa hisani ya Asif Mohiuddin

Bangladeshi inaongozwa na utawala wa kidemokrasia usiofungamana na dini yoyote, kwa hiyo hakuna sheria ya sharia wala sheria ya ukashifuji wa dini. Kama kuna yeyote anayejitangaza kuwa hamuamini Mungu, mtu huyo atakuwa na haki sawa na mwananchi wingine yeyote yule. Hata hivyo, kwa kifungu cha sheria cha 295A cha hukumu cha Bangladesh (1860), mtu yeyoye mwenye lengo la “makusudi kamili” au “kwa hujuma” “kudhuru taratibu yoyote ya kidini” atahukumiwa kwenda gerezani.

tume hiyo imetamka [23] [bn] kuwa, kwa mujibu wa Sheria ya Udhibiti wa Mawasiliano nchini Bangladesh, inaweza kuomba taarifa inayoyakiwa kutoka ka mtu yeyote au taasisi yoyote inayotumia mtandao wa intaneti. Hata hivyo, jukwaa la kublogu Amarblog [24] [bn] ilitoa tamko mnamo tarehe 22, Machi 2013 linalosema kuwa haitahatarisha haki za siri za wanablogu kufuatia agizo la serikali. Tamko liliitaka kufahamu mamlaka halali ya tume hiyo ya kuhitaji taarifa za wanablogu na pia kutaka kufahamu kama ina mamlaka ya juu ya jukwaa la Amarblog ambalo limesajiliwa nchini Uingereza na pia kumilikiwa na mfumo wa komputa wa nchi mbalimbali.

Wanablogu pia wamekuwa na mashaka kuhusiana na halali wa madai ya aina hii.

mwanablogu Mohammad Munim [25] [bn] aliipinga vikali tume hii kwenye blogu ijulikanayo kama Muktangon, ambayo ni blogu ya jamii:

বাংলাদেশের সংবিধানে মত প্রকাশের পূর্ণ মৌলিক অধিকার সকল নাগরিককেই দেওয়া হয়েছে। [..] BTRC নামের তথাকথিত স্বাধীন এই কমিশনটির হাতে যে-কোন ব্লগ বা ওয়েবসাইট বন্ধের সুইচ থাকলেও সে-সুইচের ব্যবহার দেশের সংবিধান মেনেই করতে হবে, কোন কর্তাব্যক্তির খেয়ালখুশিমতো নয়।

Kwa mujibu wa Katiba ya Bangladesh [26], kila raia ana haki ya kueleza mawazo yake kwa uhuru. […] tume iliyojipa uhuru wake yenyewe inaweza kuwa na uhuru wa kufunga mtandao au blogu yoyote, lakini wanapaswa kufanya hivyo kwa mukibu wa katiba na si kwa mujibu wa baadhi ya maofisa kwa kadiri ya watakavyojisikia.

Mwanablogu na mwanaharakati, Rayhan Rashid [27] [bn] aliandika katika ukurasa wa Facebook kuwa, serikali inaweza kuwa inatumia migogoro ya kidini ili katika harakati za kuongeza wigo wa mamlaka yake:

বিটিআরসি'র সাম্প্রতিক এই অপতৎপরতার সাথে কোথায় যেন জামাত-শিবিরের শাহবাগ আন্দোলনকে “নাস্তিকদের আন্দোলন” হিসেবে সুযোগসন্ধানী ব্র্যান্ডিংয়ের মিল আছে। জামাত-শিবিরের দরকার ছিল শাহবাগ আন্দোলনকে প্রশ্নবিদ্ধ করা, আর সে লক্ষ্যে তারা ১৯৭১ এর মতোই অস্ত্র হিসেবে বেছে নিয়েছে ধর্মীয় উম্মাদনা, আর বিভাজন-বিদ্বেষকে। সরকার বা বিটিআরসি'রও একটা সুযোগ দরকার ছিল যাকে পূঁজি করে স্বাধীন চিন্তার এই শেষ প্লাটফর্মগুলোকে কোনোভাবে নিয়ন্ত্রণের আওতায় আনা যায় – এখানেও নাস্তিকতা, ধর্মীয় অনুভুতি ব্যবহৃত হচ্ছে সুযোগসন্ধানীর অস্ত্র হিসেবে।

kuna mfanano unaopingana kati ya tamko “dhidi ya dini” lililotolewa na tume siku za hivi karibuni na “harakati za wasiomwamini Mungu” zinazosimamiwa na Jamaat-Shibir There is a striking similarity between the commission's recent “anti-religion” ban order and the branding of the Shahbag protests as an “atheist movement”. Jamaat-Shibir walitaka kuchafua harakati za Shahbag, na walifanya hivyo ili kuhamasisha mivutano ya kidini na kuhimiza utaratibu wa mgawanyiko/chuki. Tume au Serikali yawezekana ikawa imetumia nafasi hii vibaya kuamini aina fulani ya kukosekana kwa uhuru kwenye majukwaa haya ya kupazia sauti. “Msimamo wa kutokumuamini Mungu”, “unadhuru hisia za kidini”, maneno makuu yanayotumiwa kama namna ya haraka ya kujipatia nafasi fulani.

Mwanablogu Farhana Ahmed [28] [bn] alielezea katika Mukta Mona (wanaofikiri kwa uhuru), blogu katika Uhuru wa Kujieleza, sababu za kwa nini wasio mwamini Mungu na wanaharakati wasio na dini wa mtandaoni wanatafutwa:

আমার মনে হয়, এই রকম ঘটার পেছনে দুটো বিষয় কাজ করছে। প্রথমটা অনেকটা তাত্ত্বিক, নাস্তিকদের নিয়ে ধর্মব্যবসায়ী বা অ-ব্যবসায়ী দু’শ্রেণীর এস্টাব্লিসমেন্টের পক্ষের লোকজনের মনে সন্দেহ ব্যাপক। এসটাব্লিসমেন্টের স্তম্ভগুলোর মধ্যে ধর্ম অন্যতম শক্তিশালী মাধ্যম, কখনো কখনো তা রাষ্ট্রের চেয়েও শক্তিশালী, রাষ্ট্রকেই ধর্মের মদদ নিতে হয়। এসটাব্লিশমেন্টের অন্য স্তম্ভগুলোও ধ্বসে পড়ার উপক্রম হলে মদদ মাঙ্গে ধর্মের। [..] বিনা প্রশ্নে মেনে নেওয়া, অতিপ্রাকৃত শক্তির ভয়ে ভীত করে রাখা—এইসব অস্ত্র ব্যবহার করে ধর্ম তার কার্য হাসিল করে। নারী পুরুষের পুরুষতান্ত্রিক শোষণের বিরুদ্ধে সচেতন হয়ে উঠলে, ধর্মই তাকে ঠান্ডা করে; মালিকের বিরুদ্ধে শ্রমিক যেতে পারে না, কারণ আল্লা যাকে এই যামানায় কিছু দেননি, আখেরাত তো তারই জন্য। রাষ্ট্রক্ষমতায় থাকার জন্য রাজনৈতিক দলগুলোর সহজ ব্যবহার্য অস্ত্র হলো ধর্ম।

Ninafikiri kuwa kuna sababu mbili kufuatia hili. Sababu ya kwanza ni ya kinadharia, , viongozi wa Kiislam wanaoongoza kwa mabavu na Waislam wa kawaida, wote wahawakubaliani na usahihi wa wale wasioamini kuwa kuna Mungu. Dini ina nguvu sana, wakati mwingine zaidi ya wakati ambao Taifa linakubali kusaidiwa na dini. Kama miongoni mwa makundi haya yaliyo na nguvu sserikalini yakiwa kwenye matatizo, yanakuwa wakimbizi katika dini. [..] Zini zinakamilisha kazi zao kwa kuingiza imani mfu, kujichukulia vitu kw kadiri wanavyotaka wao na kuwaweka watu katika hofu. Mfumo dume unapopingwa na wanawake, dini zinawaangalia, When patriarchal oppression is protested by women, religion keeps them in check, wafanyakazi hawawezi kwenda kinyume na wafanyakazi walio na uhuru mkubwa kwani dini zinakumbusha kuwa, kwa wote walio na kidogo katika ulimwengu huu, kuna maisha yanayowasubiri mara baada ya kufa. Ili kuendelea kubakia madarakani, silaha rahisi kabisa ni dini.

Aliendelea:

দ্বিতীয় দিকটা শাহবাগের গণজাগরণ মঞ্চের প্রতিক্রিয়ার সাথে জড়িত। নাস্তিক মরলে বা মার খেলে তার প্রতি যে ঔদাসীন্য দেখাচ্ছেন আন্দোলনের সহযোদ্ধারা তাতে করে নাস্তিকরা জামাত-শিবির-হি্যবুতের সবথেকে সহজ টার্গেটে পরিণত হয়েছেন।

Sababu ya pili ni muitikio wa idadi kubwa ya watu wanaounga mkono Shahbag. Mtu anapoitwa asiye muamini Mungu, ni jambo linalohamisha hata fikra za miongoni mwa waandamanaji wenza, kwa hiyo, wale wasiomwamini Mungu wanakuwa chambo rahisi sana kwa [makundi ya siasa za kidini] Jamaat-Shibir-Hijbut Tahrir.

Update: Kwa mujibu wa taarifa za hivi karibuni [29], kamati ya watu tisa ilishiriki kwenye jukwaa la majadiliano pamoja na jamii ya viongozi wa dini nchini humo. Orodha ya wanablogu 84 na watumiaji wa Facebook imewasilishwa na kamati hiyo imeiomba jumuia hiyo kutoa ushahidi kamili dhidi ya madai yao. Kamati hiyo imeweka bayana barua pepe ambayo malalamiko kuhusiana na ukashifuji wa dini yatakapotumwa.

Makala hii ni sehemu ya makala zetu maalum za maandamano ya Bangladeshi Bangladesh's #Shahbag Protests [1]