Aprili, 2013

Habari kutoka Aprili, 2013

Uturuki: Polisi Watumia Mabomu ya Machozi Kuwatawanya AkinaMama Waandamanaji

Wafungwa wa kisiasa wa Kikurdi wamefikia siku yao ya 55 ya mgomo wa kula. Kuna mamia ya wafungwa wa kisiasa walio kwenye mgomo wa kula nchini Uturuki, na hii imesababisha maandamano mshikamano katika bara la Ulaya, na hususani ndani ya Uturuki. Mapema jana [4 Novemba 2012], wanawake ambao ni mama wa baadhi ya wafungwa wa kisiasa walifanya maandamano ya kukaa, na walijikuta wakipambana na mabomu ya machozi, pamoja na kunyunyuziwa maji ya kuwasha. Wa- Kurdi duniani kote wanapinga kimya kinachotumika kushughulikia adha yao.

Asasi za Kiraia za Urusi “Zakaguliwa” na Mwendesha Mashitaka

RuNet Echo  15 Aprili 2013

Wanaharakati wa DemVybor katika jiji kuu la eneo la Voronezh waliripoti kwenye blogu ya DemVybor[ru] kwamba Asasi Zisizo ki-Serikali zinakaguliwa na ofisi ya mwendesha mashitaka wa umma wa jiji hilo. Mashirika manne yaliyolengwa ni wanachama wa Baraza la Haki za Binadamu la Voronezh [ru]: ni Vuguvugu la Haki za Binadmau linaloendeshwa na...

Syria: Kutwiti Kutokea Vitani Jijini Aleppo

Mwandishi wa Habari Jenan Moussa amerudi mjini Aleppo, nchini Syria, akitwiti tajiriba yake wakati vita kati ya vikosi vinavyopinga serikali na vile vinavyoiunga mkono serikali inavyozidi kushika kasi. Twiti za Moussa ni za kawaida na za kibinafsi sana, zikiwapa wasomaji wake taswira ya maisha yalivyo kwa wale walio kwenye uwanja wa vita.

Vyama vya Siasa Msumbiji na Matumizi ya Intaneti

(…) kuna nafasi ambayo mpaka sasa haijatumiwa ipasavyo na vyama vya siasa nchini Msumbiji, iwe ni kwa ajili ya kueneza propaganda za kisiasa au kufanya kampeni za uchaguzi: nalo ni mtandao wa intaneti. Jukwaa la Msumbiji liitwalo Olho Cidadão (Jicho la Wananchi) lilizindua blogu mpya tarhe 2 Aprili, 2013, kwa...

Bahrain: Nani Aliyesikia Milipuko ya Bomu na Nani ni Waathirika?

Wakuu wa Serikali nchini Bahrain wametangaza leo kwamba wafanyakazi wawili wa kigeni wameuawa na wa tatu akijeruhiwa vibaya katika milipuko mitano tofauti kwenye maeneo ya Gudaibiya na Adliya, kwenye mji mkuu Manama. kwenye mtandao wa twita, habari hizi zilipokelewa kwa mashaka, kutokuamini na kusababisha mwito kwa utatuzi wa kisiasa wa kumaliza hali ya ghasia katika nchi hiyo, kufuatilia kusambaa kwa maandamano ya kuipinga serikali yaliyoanza terehe 14 Februari, 2011.

Tanzania: Ghorofa Laporomoka jijini Dar Es Salaam

Pernille anaweka picha mtandaoni zinazoonyesha ghorofa lililoporomoka jijini Dar Es Salaam, Tanzania siku ya Ijumaa, 29 Machi 20013: “Karibu kabisa na jengo hilo kuna uwanja wa kandanda unaotumiwa na watoto. Zaidi ya watu 60, pamoja na watoto, wanaripotiwa kupotea kwa mujibu wa kituo cha televisheni cha ITV. Hakuna kauli rasmi...