Misri: Mubarak ahukumiwa kifungo cha maisha

Makala haya ni sehemu ya makala zetu maalum za Mapinduzi ya Misri 2011.

Dunia ilishuhudia wakati mahakama ya Misri  ilipomhukumu aliyekuwa Rais wa zamani wa Misri Hosni Mubarak na Waziri wake wa Mambo ya Ndani Habib Al Adly kifungo cha maisha hivi leo kufuatia kukutwa na hatia ya kuhusika na mauaji ya waandamanaji.  Hukumu hiyo ilifikiwa baada ya vikao 49,  masaa 250, na kuandikwa katika kurasa 60,000, Sultab Al Qassemi
alitwiti, akimnukuu jaji Ahmed Refaat.

Hukumu hiyo ya kihistoria  ilitangazwa moja kwa moja, ikiwafanya raia wa mtandaoni kushindwa kuzuia hisia zao katika mtandao wakati vikao vya mahakama vikiendelea. Wana wawili wa kiume wa Mubarak Alaa na Gamal walifutiwa mashitaka ya rushwa, pamoja na wasaidizi wakuu wa Al Adly, walioshutumiwa kwa kuhusika na vifo vya waandamanaji wakati wa mapinduzi Misri, yalioanza Januari 25, 2011.

Kufuatia uamuzi huo, mwanablogu wa Misri Mahmoud Salem,au Sandmonkey, alitwiti:

@Sandmonkey: #ManzaYaMubarak ilikamilishwa na uamuzi bandia. Yeye na waziri wake wa ndani walipokea hukumu ya maisha gerezani ambayo yaweza geuzwa kwa urahisi, kila mmoja mwingine huru#MannzaYaMubarak

Akiongezea:

@Sandmonkey: Watu sawa ambao waliowaua na kuwatesa Wa-Misri wako huru sasa kurudia wadhifa wao katika MOI. Waza hayo#

Picha iliyotumwa katika mtandao wa twita iliyowekwa na Sultan Al Qassemi ikimwonyesha Mubarak akiwasili mahakamani asubuhi ya leo

Na Gigi Ibrahim aliripoti:

@Gsquare86: Vurumai zilizuka ndani ya hakama na umati uliimba “watu walidai uhuru wa koti elekezi” wakiimba “Ulaghai” #ManzaYaMubarak

Akiongezea:

@Gsquare86: Sielewi vipi mkuu wa MOI Aldy alishtakiwa ilhali hakuna polisi wala msaidizi wake hawakushtakiwa na lolote?!!!!#ManzaYaMubarak

Mwandishi Bel Trew alihitimisha:

@Beltrew:  Maishani gerezani kwa #Mubarak hayatakuwa mabaya kama inavyoonekana. Mule gerezani atakuwa na bustani, mahali pa kuogelea na  kiwanja cha ndegehttp://uk.reuters.com/article/2012/06/01/uk-egypt-trial-mubarak-idUKBRE85017O20120601 #ManzaYaMubarak

Mwandishi Patrick Tombola alidondoa:

@ptombola:  Mubarak na Adly walihukumiwa kwa kutozuia mauaji na kutokutoa amri ya kuzuia mauaji yaliyotokea. Tofauti kubwa na isiyo ya kuvumilia.#Misri #ManzaYaMubarak

Lakini Mina Zekri anatukumbusha [ar]:

نذكر الجميع قبل الحكم أنه سيكون حكما ابتدائيا والعبرة بحكم محكمة النقض بعدما يطعن المتهمون على الحكم ‎‫#محاكمة_مبارك‬‏ ‎‪#mubaraktrial
@minazekri: Ningependa kuwakumbusha nyinyi wote kwamba uamuzi huu ni uamuzi wa mwanzo tuu na twapaswa tungoje koti ya rufaa baada ya washtakiwa kukata rufaa dhidi ya uamuzi.

Asteris Masouras anaonyesha mchoro wa miitikio ya watumiaji wa mtandao wa twita hapa. Na Rayna St. anakusanya miitikio mingine katika mkusanyiko uitwao Storify hapa. Noon Arabia pia anaonyesha miitikio hapa.

Kwa maoni zaidi, angalia #Mubaraktrial ambayo ni alama habari inayokusanya habari hizo katika mtandao wa twita.

Makala haya ni sehemu ya makala zetu maalum za Mapinduzi ya Misri 2011.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.