- Global Voices in Swahili - https://sw.globalvoices.org -

AZISE ya Uwazi Yajiandaa kwa Uchaguzi wa Jumapili Nchini Venezuela

Mada za Habari: Amerika Kusini, Venezuela, Teknolojia, Uandishi wa Habari za Kiraia, Uchaguzi, Mtandao wa Teknolojia na Uwazi

Katika siku chache zijazo, wapiga kura wa Venezuela wataingia katika uchaguzi kwa mara ya pili [1] ndani ya miezi sita. Watakuwa wakimchagua mrithi wa rais wa zamani wa nchi hiyo Marehemu Hugo Chavez, alifariki dunia/a> mwezi Machi. Mwelekeo wa kisiasa nchini humo ni tete kuliko ilivyokuwa wakati wa uchaguzi [2] wa Oktoba, ingawa hata hivyo kikundi cha Asasi zizizo za Kiserikali zimekusanya nguvu za pamoja ili kushughulikia suala la uwazi katika mchakato wa uchaguzi huo.

Kwa hakika ni mazingira ya siasa zilizopoozwa nchini Venezuela zinafanya ushirikiano huu kuwa wa kutazamwa. Elección Ciudadana – jina la mwamvuli wa kikundi hicho – liliibuka [3] mwezi Oktoba kupitia juhudi za asasi inayoitwaVenezuela Inteligente [4] [es], ana imetumia miezi mitano kutengeneza ushirikiano mpana baina ya mashirika. Kwa kutumia mahusiano haya za ziasa, mashirika yanataraji kuweza sasa kuifikia hadhira kubwa zaidi ya raia wa nchi hiyo. Kama mwakilishi wa mmoja wapo ya wanachama wa muungano huo, Transparencia Venezuela [5] [es], walisema:

Lengo letu ni kuweka huduma ya mifumo mbalimbali ya mawasiliano kadiri inavyowezekana kwa watu ili wawezi kufikisha malalamiko yao kwa kutumia mifumo inayowafaa zaidi, wakati kampeni zinazoanza kwesho na hata siku ya uchaguzi.

Transparencia Venezuela (@NoMasGuiso [6]) [es] pia walitwiti:

@NoMasGuiso [7]: Tu denuncia con la de otros puede hacer la diferencia, no te quedes callado y denuncia los abusos que veas en estas elecciones #NoMasGuiso [8] (hakuna ufisadi tena)

@NoMasGuiso [7]: Taarifa yako na za wengine zinaweza kuleta tofauti, usikae kimya – toa taarifa za kuvurugwa kwa taarifa kadri unavyoziona katika uchaguzi huu. a href=”https://twitter.com/search?q=%23NoMasGuiso&src=hash”>#NoMasGuiso

Je, juhudi hizi za kuwafikia wa-Venezuela wengi zaidi kwa ujumbe rahisi tu kuwa watu wanaweza kupata na kutuma habari/taarifa kuhusiana na mwenendo wa uchaguzi zitafanya kazi? Mwanachama mwingine wa ushirikiano huo, Usted Abusó, wamepokea zaidi ya ripoti 200 ndani ya mwaka 2013 ambazo sana zinahusiana na matumizi ya rasilimali za nchi kwa minajili ya kisiasa.

Elección ciudadana map [9]

Ramani ya Elección ciudadana

Karibu ripoti 200 zimeletwa mpaka sasa kwa Elección Ciudadana, ambao nao wanatoa ramani [9] [es] ambayo zinatokana na habari za wananchi zilizokuwa zimetumwa kwa ushirikiano na mashirika. Timu yake inatarajia kupokea taarifa zaidi mwisho wa juma hili, ambapo matukio ya matumizi ya nguvu, ukamataji na hata kushindwa kufanya kazi kwa mifumo ya uchaguzi yanauwezekano mkubwa wa kutokea. Kwa hakika, matumizi ya nguvu kwa malengo ya kisiasa yameanza -kwa mfano kuna mauaji [10] [es] yanayoonekana kuwa na msukumo wa kisiasa pamoja na lugha za matusi [11] [es] juma hili.

Katika siku ya uchaguzi, Elección Ciudadana wataendesha kituo cha kujitolea – kilichoratibiwa kwa kiasi kikubwa na Venezuela Inteligente [4] [es] – mahususi kwa ajili ya watu binafsi kupokea, kuhakiki na kuchapisha taarifa. Watu wengine wengi watakuwa wakijitolea kutokea nyumbani. Tumaini lao kubwa ni kuwa mitandao iliyohakikiwa na tajiriba (uzoefu) za mwanachama wa muungano huo vitarahisisha mchakato, kuzijumlisha na kuzijibu taarifa wakati wa siku ya uchaguzi; watakuwa wakijaribu kutazma miitikio kutoka katika vyombo vikuu vya habari pamoja na mamlaka rasmi ya uchaguzi [12][es].