28 Aprili 2013

Habari kutoka 28 Aprili 2013

Serikali ya Bangladeshi Yawafuatilia Wanablogu, Yawatuhumu Kuukashfu Uislam.

  28 Aprili 2013

Kadri mapambano makali kati ya wanaharakati wa Kiislamu na serikali yanavyoendelea kusababisha migongano ya kidini nchini Bangladesh, Mamlaka ya Mawasiliano ya nchi hiyo imechukua hatua ya kuwanyamazisha wanablogu wanaoonekana wapinzani wa Uislamu na serikali. Asif mshindi wa tuzo ya mwanablogu bora amekuwa akilengwa na hatua hizo kwa siku za hivi karibuni.

Uganda: Kukumbuka milipuko ya mabomu ya 2010

Wananchi wa Uganda wameutumia mtandao wa Twita na Facebook kuwakumbuka wahanga 2010 wa milipuko yha mabomu iliyotokea kwenye klabu ya Rugby huko Kyaddondo na katika baa ya Kijiji cha Kiethiopia jijini Kampala Uganda.Mashambulizi hayo yalitokea wakati ambao wapenzi wa kandanda walikuwa wakitazama mpambano wa fainali kati ya Uhispania na Uholanzi uliofanyika nchini Afrika Kusini.