Habari kutoka 13 Aprili 2013
Syria: Kutwiti Kutokea Vitani Jijini Aleppo
Mwandishi wa Habari Jenan Moussa amerudi mjini Aleppo, nchini Syria, akitwiti tajiriba yake wakati vita kati ya vikosi vinavyopinga serikali na vile vinavyoiunga mkono serikali inavyozidi kushika kasi. Twiti za Moussa ni za kawaida na za kibinafsi sana, zikiwapa wasomaji wake taswira ya maisha yalivyo kwa wale walio kwenye uwanja wa vita.
AZISE ya Uwazi Yajiandaa kwa Uchaguzi wa Jumapili Nchini Venezuela
Wakati wapiga kura wa Venezuela wakijiandaa kuelekea kwenye uchaguzi wa mara ya pili katika kipindi cha miezi sita, kikundi cha Asasi Zisizo za Kiserikali kimekusanya nguvu ili kuhakikisha kuwa wanakuza uwazi katika mchakato wa uchaguzi.