Unaona lugha zote hapo juu? Tunatafsiri habari za Global Voices kufanya habari za kidunia zimfikie kila mmoja.

Wa-Mauritania Wapinga Udhalilishaji wa Viwanja vya Tahrir Square

صورة من الوقفة نشرها حساب موريتانيا اليوم على فيسبوك

Mwandamanaji akisema “Tunapinga Udhalilishaji” picha ya Jarida la “Mauritania Today” kwenye mtandao wa Facebook.


Siku ya Jumanne Februari 12, 2013, kikundi cha wanaharakati wa ki-Mauritania kiliandaa [ar] maandamano mbele ya Ubalozi wa Misri jijini Nouakchott, mji mkuu wa Mauritania, kupinga udhalilishaji wa kijinsia na ubakaji ambao wanawake wa ki-Misri wamekuwa wakikumbana nao kwenye viwanja vya Tahrir jijini Cairo.

Tukio hilo la maandamano liliratibiwa na “Etkelmi” (Sema kwa kiarabu) [ar – fr], Asasi Isiyo ya Kiserikali inayopambana na ubakaji nchini Mauritania. Mekfoula Brahim anawapa heshima wale wote walioshiriki maandamano hayo [ar]:

شكرا لكم يا مواطنو ا العالم على وقفتكم امام السفارة المصرية فى انواكشوط لدعم نساء مصر اللائى يمارسن حقهن فى التظاهر السلمى فى مصر وعلينا جميعا القيام بوقفة اخرى احتجاجا على دعم الارهاب علنا من طرف الكثيرين والتأصيل له فى ثقافتنا المنفتحة

Asante sana wananchi wote duniani kote kwa kuandamana mbele ya Ubalozi wa Misri jijini Nouakchott kuwaunga mkono wanawake wa Misri wanaotumia haki yao ya kuandamana kwa amani nchini Misri. Tuanze kuandaa mandamano mengine kuwapinga wale (wengi) wanaounga mkono ugaidi na wale wanaojaribu kuuchukua utamaduni wentu wa uwazi.

Uwanja wa Maoni Umefungwa