- Global Voices in Swahili - https://sw.globalvoices.org -

Ramani za Mpaka wa Kikoloni wa Sudan Kusini Ziko Wapi?

Mada za Habari: Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara, Sudani Kusini, Historia, Siasa, Uandishi wa Habari za Kiraia

Joseph Edward anazungumzia [1]kupotea kwa ramani za mpaka wa Sudan Kusini za enzi za ukoloni: “Majadiliano yameibuka kuhusu ramani ambazo zilidaiwa kuchukuliwa na Waingereza baada ya Sudan kupata uhuru mnamo mwaka wa 1956. Huku baadhi a watu wanaamini kwamba nyaraka hizo za kihistoria zinaweza kupunguza migogoro ya mpaka inayoendelea, watafiti wanatilia shaka uwepo wa ramani hizo.