- Global Voices in Swahili - https://sw.globalvoices.org -

Vurugu Zinazofadhiliwa na Serikali Nchini Angola

Mada za Habari: Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara, Angola, Haki za Binadamu, Uandishi wa Habari za Kiraia, Wanawake na Jinsia

Mwanablogu Claudio Silva anaandika kwenye [1] makala yake Africa Ni Nchi kwamba mtazamo wa kina juu ya vurugu zinazofadhiliwa na serikali (kufukuzwa watu mijini na kupigwa kwa waandamanaji) unahitajika ili kuelewa video mbili zilizosambaa sana mtandaoni na kuleta sintofahamu kubwa nchini (tazama habari maalumu za Global Voices [2]). Anaandika “vurugu za Angola zimetoka ngazi za juu: Serikali”.