- Global Voices in Swahili - https://sw.globalvoices.org -

Uhuru wa Vyombo vya Habari Nchini Myanmar Bado ni Giza

Mada za Habari: Asia Mashariki, Myanmar (Burma), Uandishi wa Habari za Kiraia, Uhuru wa Kujieleza, Vyombo na Uandishi wa Habari

Uamuzi wa Myanmar wa kuivunja [1] bodi katili ya ukaguzi ulisifiwa na makundi mbalimbali ya watu kuwa ni hatua ya kuelekea kuimarisha uhuru wa vyombo vya habari nchini Mynmar. Lakini wafuatiliaji wa uhuru wa vyombo vya habari waliainisha vitisho vinavyoendelea, changamoto na mashambulizi waliyokwisha kuyapata waandishi wa habari waishio nchini Myanmar kwa mwaka uliopita.

Kwa mfano, waandishi wa habari wa kujitegemea wanaendelea kuwa katika hali ya hatari ya kukumbwa na vifungu mbalimbali vya sheria kama wataweka bayana hali ya sintofahamu katika uongozi au kuwakosoa viongozi wa ngazi za juu serikalini. Mnamo tarehe 7 Februari, 2013, bunge la Mynmar liliunda tume ya kumchunguza wandishi kufuatia makala iliyoandikwa kwenye blogu iliyokuwa na kichwa cha habari “Juu ya Sheria [2]” [my]. Makala iliandikwa na mtu aliyetumia jina la kubuni “Dr. Sate Phwar” kwenye blogu ya Sauti ya Myanmar (Voice of Myanmar) [3] [my]. Makala hiyo iliwakashifu wabunge kwa kutoizingatia katiba na pia kwa kujifanyia maamuzi bila kuzingatia ushauri wa Rais. Aliandika kwa kejeli:

Kwanini msiongeze marekebisho haya mapya kwenye katiba ambayo kwa vyovyote ambavyo katiba itaelekeza, mwenyekiti wa Bunge na wenzake wanaweza kuamua wao wenyewe kwa kupiga kura Bungeni.blockquote>

[4]

Picha iliwekwa na iFreedom Media Group (Burma) [4] ambalo liliandika kuwa mwandishi wa habari ashambuliwa na wavamizi wa ardhi kwenye makazi yake mapya. Taarifa hiyo fupi iliongeza pia kuwa, “baadhi ya taarifa, zinasema kuwa, huu ni mpango ulioandaliwa na kikosi maalum cha polisi ili kuwafanya watu wawachukie wavamizi wa ardhi.”

Sambamba na hili, mwaka uliopita, jarida la nchini MyanmarThe Voice Weekly [5] lilituhumiwa [6] na wizara ya madini kwa kuikashifu pale jarida hili lilipotoa taarifa za wizara hii kuwa inatumia vibaya fedha pamoja na udanganyifu mwingine. Kwa bahati nzuri, wizara ilitupilia mbali [7] tuhuma hizi mapema mwaka huu.

Siku za hivi karibuni, waandishi wa habari, walipokea [8] [my] angalizo kutoka katika kampuni ya Google kuwa yawezekana kukawa na mashambulio yaliyo andaliwa kutoka kwa “ washambuliaji waliofadhiliwa na serikali”. Angalizo hilo lilitolewa mara baada ya kurasa za Facebook za jarida la kujitegemea nchini Myanmar la The Voice Weekly [5] [my] na Eleven Media Group [9] [my] kuharibiwa nakikundi kinachojiita “Myanmar isiyojulikana”. Hata hivyo, serikali imekanusha [10] kujihusisha kwa namna yoyote na shambulizi hili la uharibifu wa taarifa katika mtandao wa intaneti.

Labda kwa kuzingatia hujuma kwenye tovuti za habari, tovuti maalum [11] [my] ya Rais wa Myanmar ilishambuliwa mnamo Februari 5, 2013 na wavamizi walioshukiwa [12] kuwa ni wa kikundi kinachojulikana kwa jina la “Indonesian Fighter Cyber”.

Pia, ni kawaida sana kukuta makundi ya watu wenye hila, picha za kupotosha na jumbe mbalimbali kwnye mitandao ya kijamii. Wakati wa machafuko ya Rakhine [13] mwaka 2012, picha za upotoshaji kutoka pande zote mbili za mgogoro zilisambaa kwenye mtandao wa intaneti.

Wakati huo huo, Taw Win Daund [14] aliweka picha [15] katika ukurasa wake wa Facebook ambayo inadhaniwa kuwa ni picha ya watoa maoni waliokodishwa. Picha hiyo aliipa kichwa cha habari:

Picha imewekwa na Taw Win Daund [15]

Watoa maoni waliokodishwa au wanafunzi wa mafunzo ya kijeshi? Picha imewekwa na Taw Win Daund

Watoa maoni waliokodishwa, wanahamasisha vurugu kati ya Rais Thein Sein na Makamu Mkuu wa Majeshi Min Aung Hlaing kwa kuandika maoni ya kejeli mwishoni mwa makala katika majarida ya Eleven Media, the Voice Weekly na 7 Days News journal.

Kuna mitazamo tofauti katika picha hii. Steven Myo [16] aliandika:

Waandishi wanahusisha hata wale waliopata mafunzo huko Urusi.

La Min Aung [17] alikanusha madai hayo:

Hii siyo sahihi, kutumia picha ya wanafunzi katika chuo cha mafunzo ya kijeshi ili kupotosha siyo vizuri. Hii itapelekea mgogoro miongoni mwa watu na pia katika jeshi.

Pamoja na kuwa ni vigumu kusema kama ni ukweli au sio mkweli, maoni ya kukejeli [18] na matumizi ya lugha chafu ni kawaida sana katika kurasa za Facebook nchini Myanmar.