- Global Voices in Swahili - https://sw.globalvoices.org -

“Wanasemaje Bamako?” Mazungumzo na Awa anayeishi Mali

Mada za Habari: Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara, Mali, Ufaransa, Filamu, Harakati za Mtandaoni, Uandishi wa Habari za Kiraia, Vita na Migogoro, Wanawake na Jinsia
[1]

Mazungumzo ya kila siku kwa njia ya skype(kwa Kifaransa)  kati ya Awa Traoré aliyeko Bamako na Anne Morin akiwa Ufaransa (kupitia anuani ya @annagueye)

Anne Morin na Awa Traoré wanabadilishana mawazo kuhusiana na maisha ya kila siku mjini Bamako, ujira usiokidhi mahitaji [2], gharama za maisha na hali ya kisiasa isiyotabirika [3] wakati huu ambapo vita vinanukia nchini humo.