- Global Voices in Swahili - https://sw.globalvoices.org -

Rais wa Chadi Awateua Wanawe Kushika Nafasi Nyeti

Mada za Habari: Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara, Chad, Habari za Hivi Punde, Siasa, Uandishi wa Habari za Kiraia, Utawala

Djamil Ahmat anaripoti kuwa rais Déby [1] wa Chadi amemteua mwanae wa kiume Mahamat Idriss Déby, 24, kuwa brigedia jenerali [2] [fr] pamoja na maafisa wengine wanne. Tchadanthopus anaongeza kuwa mwanae mwingine Zackaria Idriss Deby alisemekana kukabidhiwa umakamu wa rais [fr]  [3] nafasi ambayo inampa madaraka yote wakati baba yake anapokuwa nje ya nchi.