Rais wa Chadi Awateua Wanawe Kushika Nafasi Nyeti
Lova Rakotomalala Christian BwayaAfrika Kusini mwa Jangwa la Sahara
Djamil Ahmat anaripoti kuwa rais Déby wa Chadi amemteua mwanae wa kiume Mahamat Idriss Déby, 24, kuwa brigedia jenerali [fr] pamoja na maafisa wengine wanne. Tchadanthopus anaongeza kuwa mwanae mwingine Zackaria Idriss Deby alisemekana kukabidhiwa umakamu wa rais [fr] nafasi ambayo inampa madaraka yote wakati baba yake anapokuwa nje ya nchi.