- Global Voices in Swahili - https://sw.globalvoices.org -

Msumbiji: Uhamasishaji wa Kiraia Kuwasaidia Waathirika wa Mafuriko

Mada za Habari: Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara, Msumbiji, Harakati za Mtandaoni, Majanga, Uandishi wa Habari za Kiraia

sos chokwe [1]

Baada ya mvua kubwa iliyosababisha mafuriko kusini mwa Msumbiji yaliyowaacha maelfu ya raia bila makazi na wengi kupoteza maisha, kikundi cha kiraia cha Msumbiji Makobo [2] kimeanza kampeni ya mshikamano inayoitwa “S.O.S. Chókwè [1]” kukusanya misaada ya hisani kwa ajili ya waathirika.