- Global Voices in Swahili - https://sw.globalvoices.org -

Mashoga Washambuliwa Kaskazini mwa Kameruni

Mada za Habari: Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara, Kameruni, Dini, Haki za Binadamu, Haki za Mashoga, Uandishi wa Habari za Kiraia

Oscarine Mbozo’a anaripoti [1] [fr] katika blogu ya L'Actu kuwa shoga mmoja akiwa ameambatana na mwenzi wake walizomewa karibu na soko mnamo tarehe 6, Januari 2013, mjini Maroua, Kaskazini mwa Kameruni:

Goche Lamine, mfanyabiashara wa madawa, alikamatwa na mwanafunzi wa shule ya sekondari aitwaye Sanda, mwenye umri wa miaka 17. Umati wa watu uliokuwepo sehemu hiyo baada ya kugutushwa na mtoto aliyekuwa akipiga kelele “samaroka! Samaroka (yaani mashoga katika lugha ya ki-Fulfulde), uliwakimbilia watu hao na kuanza kuwarushia mawe.