- Global Voices in Swahili - https://sw.globalvoices.org -

Jukwaa la Kiafrika Lenye Makala za Bure za Kitaaluma

Mada za Habari: Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara, Kenya, Elimu, Teknolojia, Uandishi wa Habari za Kiraia
[1]

Video inayoonesha namna www.hadithi.org inavyofanya kazi kuboresha upatikanaji wa zana za utafiti kwa Afrika

Januari 24, ni siku ambayo inategemewa kuwa ya kuzindua rasmi Hadithi [2], ambalo ni jukwaa la kuhifadhia [3] zana za bure za kitaaluma mjini Nairobi, Kenya. Wasomi mbalimbali na wadau wa mitandao watakusanyika pamoja kujadili upatikanaji wa zana huru za kitaaluma katika elimu ya juu nchini Kenya. Hadithi itasaidia kutafuta, kuona na kushusha makala kutoka katika taasisi za kitafiti duniani kote. Kujiandikisha kwa tukio hili, itafute Hadithi mtandaoni kupitia Facebook [4] na tovuti ya Eventbrite [5].