- Global Voices in Swahili - https://sw.globalvoices.org -

Video ya Kuomba Ujenzi wa Vyoo vya Umma huko Jharkhand, India

Mada za Habari: Asia ya Kusini, India, Haki za Binadamu, Maandamano, Maendeleo, Uandishi wa Habari za Kiraia, Utawala

Amit Topno, mwakilishi wa jumuiya ya hiari “inayopiga picha za video” [1] aliripoti kwamba wakati wa kijiji cha Nichitpur katika Jimbo la Jharkhand hawana choo chochote cha umma kinachotumika. Wanavijiji wanaziomba mamlaka za serikali za mitaa kupitia video hii [2] kuhakikisha kuwa vyoo vinavyostahili matumizi ya binadamu vinajengwa.