Mwanablogu wa Iran Sattar Beheshti Ateswa hadi Kufa

Picha zilizopigwa kutoka katika blogu ya Sattar Beheshti http://magalh91.blogspot.se

Watumiaji wa mtandao wa intaneti wa nchini Iran wameanzisha vurugu kubwa mtandaoni [fa] baada ya kupata habari ya kusikitisha ya kifo cha mwanablogu aliyefia gerezani iliyowekwa kwa mara ya kwanza mtandaoni [fa] na tovuti za upinzani. Kwa mujibu wa mahojiano na watu wa wafimilia ya Sattar Beheshti na pia taarifa kutoka katika tovuti za haki za binadamu, mwanablogu huyu alikamatwa mnamo tarehe 28 Oktoba, 2012 na takribani siku kumi baadae, alitangazwa kuwa amefariki.

Sattar Beheshti. Chanzo: Kampeni katika Facebook kwa ajili ya Sattar Beheshti

Wafungwa 41 wa kisiasa bravely walichapisha[fa]kwa weledi mkubwa taarifa iliyokuwa inasema walishuhudia dalili za kuteswa katika mwili wa Sattar.

Mashirika mbalimbali ya kimataifa ikiwa ni pamoja na waandishi wa habari wasio na mipaka maalum wameishinikiza mamlaka ya Iran kutoa ufafanuzi wa kina wa mzingira ya kifo cha mwanablogu huyu na kuzitaka jamii za kimataifa kutokukubali kosa hili kumalizwa bila ya wahusika kuadhibiwa.

Uanaharakati wa mawsiliano wa Beheshti, ikiwa ni pamoja na blogu [fa] yake mwenyewe umeonekana dhahiri kuwa ndio uliompelekea kuwekwa kukamatwa kikatili, kuteswa na hatimaye kuuawa akiwa na umri wa miaka 35. Kauli mbiu ya Blogu yakeiliyotafsiriwa kutoka katika lugha ya Farsi inasomeka: “Ukosoaji. Maisha Marefu kwa Watu wa Iran na Iran. Maisha yangu kwa ajili ya Iran.” Makala yake ya mwisho kuiweka ilikuwa tarehe 26 Oktoba. Alikamatwa siku mbili baadae.

Katika makala yake ya mwisho, alimkosoa Ali Larijani, kiongozi wa bunge la Iran. Alisema kuwa, Larijani na jamhuri ya Kiislamu ni wanafiki katika kuzikosoa nchi nyingine kwa kukiuka haki za binadamu. Beheshti aliandika [fa]:

Unaongelea kuhusu ukiukwaji wa haki za binadamu nchini Saudi Arabia, Bahrain….. nchi za Magharibi, kama vile mliiumba mbingu katika ardhi ya Iran. Haukufanya hivyo. Kama kweli uliiumba hii mbingu, kwanini usingewaita watu nchini Iran waje waione?

Watumiaji wa mtandao wa Iran wameonesha hisia zao kufuatia kosa hili la “jinai” linalotukumbusha kwa mara nyingine tena kuwa wanablogu wanaweza kuishia kutoa maisha yao sadaka kwa kazi zao zilizo na tija.

Ukurasa wenye kichwa cha habari kisemacho “ Wale waliohusika katika kifo cha Sattar Beheshti wanapaswa kuwekwa hatiani” [fa] ulianzishwa Facebook .

Ahmad Sharifi (@sharifi123) alitwiti:

وبلاگ نویس مملکت رو گرفتن به جرم وبلاگ نویسی تو زندان اوین کشتن. بعد رییس جمهور مملکت رفته اجلاس جهانی دموکراسی از دموکراسی غرب انتقاد میکنه

Walimchukua mwanablogu huyu kutoka rumande na kwenda kumuulia gerezani, na halafu Rais huwa anahudhuria Mkutano wa Dunia wa Demokrasia nchini Indonesia na kukosoa demokrasia ya Magharibi.

Hasan Ejraei aliweka makala katika Google+ wasifu wake [fa]:

Ni kitu gani kinaendelea huko kiasi kwamba kila wakati ni lazima mtu auliwe?. Wanawafanyia nini watu katika rumande zao? Walimfanyia nini Zahra Bani Yaghoub hadi wakamuuwa? Walimfanyia nini Zahra Kazemi hadi wakamuuwa? Wanawafanyia nini na wengine wote ambao bado wapo rumande? Mahakama lazima iwajibike kwa hili. Hawahusiki? Sawa, hawakupaswa. Ninaomba msamaha.

Miaka mitatu iliyopita, mwanablogu mwingine, Omid Reza Mir Sayafi alifariki ndani ya gereza la Iran katika mazingira ya kutatanisha.

2 maoni

jiunge na Mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.