- Global Voices in Swahili - https://sw.globalvoices.org -

Korea Kusini: Mpango wa Kuwakutanisha Wenzi Wakwama

Mada za Habari: Asia Mashariki, Korea Kusini, Sanaa na Utamaduni, Uandishi wa Habari za Kiraia, Wanawake na Jinsia

Mpango mpya kabisa wa kuwakutanisha wenzi kwa njia rahisi [1] katika mkesha wa Krismas nchini Korea Kusini hatimaye ulijikuta ukishindwa kabisa baada ya waliojitokeza asilimia 90 kuwa ni wanaume. Inasemekana zaidi ya watu 20,000 walijiandikisha na hata polisi walikuwepo kufuatia uwezekano wa vitendo vya ngono za kulazimisha. Mtumiaji mmoja wa mtandaoalibainisha [2] [ko] ukweli kwamba kosa lilikuwa ni kile alichokichagua mwanaume ndicho kilichosababisha kushindikana kwa zoezi hilo la kuwakutanisha wenzi.