- Global Voices in Swahili - https://sw.globalvoices.org -

Mwanzilishi wa Kikundi cha Kijeshi Kilichofutwa Nchini Pakistani Ajitolea Kuisaidia Marekani.

Mada za Habari: Uandishi wa Habari za Kiraia

Baada ya kusababisha uharibifu mkubwa pembezoni mwa pwani ya atlantiki nchini Marekani, Kimbunga kikubwa sandy [1] kinachukuliwa kama kimbunga kilichosababisha madhara makubwa ambayo hayakuwahi kutokea. Kiasi cha fedha kinachokadiriwa kufikia dola za kimarekani milioni 45 [2] zinahitajika ili kurekebisha na kujenga upya makazi na miundombinu, ambapo nchi inajiandaa kukabiliana na hasara hiyo. Watu wasiopungua 33 inaelezwa kuwa wamepoteza maisha [3] na idadi kubwa ya watu wameachwa bila makazi katika maeneo mbalimbali ya pwani ya Mashariki.
Huku kimbunga hiki kikiendelea kuleta madhara, Hafiz Mohammad Saeed, mwanzilishi wa kundi la kijeshi lililofutwa, Lashkar e Taiba (LeT) na kiongozi wa Jaamat ud Dawa (JuD) alitoa msaada wa kibinadamu [4] kwa nchi ya Marekani ili kuisaidia kufuatia uharibifu uliotokea.

[5]

Kimbunga Sandy kilichosababisha uharibifu mkubwa ulioenea sehemu za mwambao na pwani ya Queens. Wengi wamepoteza makazi yao, biashara na mali zao. Picha na Kevin Downs. Haki miliki na Demotix.

Akiahidi kusaidia kwa hali na mali misaada ya kila aina, alisema, “Jamaat-ud-Dawa iko tayari kutuma watu wa kujitolea, madaktari, vyakula, madawa na vitu vingine vya kuwasaidia wahanga endapo serikali ya Marekani itaturuhusu”.

Akijulikana kama muongozaji mkuu wa mashambulizi ya Mumbai ya mwaka 2008, mwanzilishi wa JuD pia alitoa msaada wa dola milioni 10 za kimarekani [6].

Hata hivyo, ubalozi wa Marekani katika mji mkuu wa Islamabad nchini Pakistani umekataa kupokea msaada kutoka kwa Saeed. Wakitumia ukurasa wao wa Twita, ubalozi huo umeweka bayana kuwa pamoja na kuwa wanathamini kitendo cha waislamu kutoa misaada, hawakutilia maanani kabisa msaada wa ndugu Saeed.

@usembislamabad [7] (Ubalozi wa Marekani Islamabad): Tunaheshimu utamaduni wa Waislamu wa kutoa misaada kwa wahitaji, lakini hatuwezi kutilia mkazo msaada wa Hafiz Saeed.

Kufuatia maelezo hayo katika Twita, msemaji wa JuD alijibu kama ifuatavyo:

@JuD_Official [8] (Jamat ‘ud’ Da'wah): @usembislamabad Tulitoa msaada wetu wa dhati kutokana na hali halisi ya janga. Ni matarajio yetu kuwa Waislamu wanaoishi Marekani watauendeleza utamaduni huu. Inshallah

@JuD_Official [9] (Jamat ‘ud’ Da'wah) @usembislamabad Msaada wetu ni kwa ajili ya watu wa Marekani, tutawahusisha Waislamu wa Marekani kuwa mstari wa mbele katika kuwasaidia ndugu zao.

@JuD_Official [10] (Jamat ‘ud’ Da'wah): @usembislamabad Rajiv Shah kutoka shirika la Kimarekani la kutoa misaada alitoa kipao mbele kwetu pale alipotembelea kambi yetu ya kutoa misaada mwaka 2010 na kutoa misaada – #Hafiz Saeed

Ubalozi wa Marekani ulienda mbali pale walipomuhusisha Saeed na tuhuma za kujihusisha na mashambulizi ya Mumbai na pia kuliita shirika lake JuD kuwa ni shirika lililo na mrengo wa kigaidi.

@usembislamabad [11] (US Embassy Islamabad ‏): Saaed anatafutwa kuhusishwa na mashambulizi ya Mumbai yaliyopelekea watu 166 kuuawa. JuD ni shirika linalotambuliwa na Umoja wa Mataifa na Marekani kuwa ni la Kigaidi.

Ukurasa wa Twita wa JuD ulikuwa tayari kutoa majibu.

@JuD_Official [12] (Jamat ‘ud’ Da'wah): @usembislamabad Serikali ya Marekani imekubali ukweli ambao haukudhibitishwa kuwa ni sahihi ndidi ya Hafiz Saeed. Kauli ya UNSCR bado inasubiriwa. Hakuna kinachoachwa.

Maoni kuhusiana na msaada huu bado yanakanganya.

@Rifaqat_Mir [13] (Rifaqat A. Mir): pamoja na uadui unaowekwa na Marekani kwa Hafiz Saeed, bado ana nia ya dhati ya kutoa misaada katika kuendelea kuonesha kumjali adui yake.

@humayusuf [14] (Huma Yusuf): wanasema kuwa Waislam hawana roho ya huruma, lakini utayari wa Hafiz Saeed wa kuwasaidia wahanga wa kimbunga cha Sandy inaonekana ni kichekesho. http://www.thenews.com.pk/Todays-News-13-18499-Hafiz-Saeed-offers-humanitarian-aid-to-US …

@anDYRude [15] (Anirudh Malladi): Punde tu nimesoma kuwa, Hafiz Saeed, gaidi aliyeogopeka, amejitolea”kutoa msaada wa vyakula, madaktari, n.k ” kwa wahanga wa kimbunga cha sandy. LMAO!

@nidak_ [16] (Nida Khan): Kuvumilia jumbe za kashfa zinazoendelea kati ya Hafiz Saeed na ubalozi wa Marekani mjini Islamabad ni 1-1, ningeweza kusema. #Mzunguko unaofuata?

@anamzehra86 [17] (Anam Zehra): Majibu ya Ubalozi wa Marekani kufuatia kujitolea kwa Hafiz Saeed ni namna yao ya kutaka kusema kuwa, ”tunachukulia dini yako kwa uzito mkubwa sana, nawe ungalipaswa pia kufanya hivyo”