Chile: Mahabusu wa Mapuche Wamaliza Mgomo wa Kutokula Uliodumu kwa Siku 60

Vijana wawili wanaume, wazawa wa jamii ya Mapuche kutoka Chile ya Kusini, mnamo tarehe 13 Agusti, 2012 walihukumiwa siku 541 za kukaa gerezani kufuatia kuhusika na shambulio dhidi ya polisi katika machafuko yaliyotokea tarehe 2 Novemba, 2012 katika sehemu ya vijijini ya jamii ya Ercilla .

Paulino Levipán mwenye umri wa miaka 19 na Daniel Levinao mwenye umri wa miaka 18 walianzisha mgomo wa kutokula mnamo tarehe 27, wakishirikiana na Rodrigo Montoya Melinao na Eric Montoya Montoya ili kupinga kukamatwa kwao. Waliotangulia kutajwa walituhumiwa kwa kumuua polisi aliyekuwa aliyekuwa doria katika shamba la wanyama lijulikanalo kama Centenario katika eneo la jumuia hiyo ya Ercilla mapema mwezi Augusti 2011. Watu hawa wamekuwa wakihojiwa mara kwa mara.

Jana, Oktoba 25, wafungwa wanne wa gereza la mapuche waliamua kusitisha kususia kula mara baada ya Mahakama Kuu ya Chile kukubaliana na baadhi ya matakwa yao. Tayari wapo katika kituo cha matunzo cha gereza hilo wakipata mlo.

Kinakilishi (Stencil) cha Mapuche, picha na mtumiaji wa Flickr aitwaye Paul Lowry (CC BY-NC-ND 2.0)

Mahakama kuu ya Chile ilisimamia katika kuharakisha uchunguzi uliopelekea hukumu yao. Katika shauri laDaniel, uchunguzi mwingine uliagizwa kufanyika kwa kuwa ule wa kwanza ulikosa ushahidi wa kutosha ili kukamilisha hukumu.a. kama ilivyo kwa Paulino, mahakama ilibadilisha shitaka lake na kulifanya kuwa ni la kujeruhi kwa kuzingatia “makosa ya kiushahidi katika matumizi ya sheria”, hivyo hukumu yake ikabadilishwa kutoka miaka 10 gerezani hadi kifungo cha nje ya gereza kwa miaka 3.

Msimamo wa sasa wa serikali

Rais Sebastián Piñera alizungumzia mgomo wa kutokula [es] wakatialipotembelea jamii ya watu wanoishi pamoja ya Ercilla mapema mwezi Oktoba, aliporejelea sera ya muda mrefu kuhusiana na migogoro ya jamii hizi:

¿Vamos a permitir que ese intento de homicidio quede impune? La justicia llegó a un fallo definitivo y por tanto pienso que si ellos cometieron un delito, la huelga de hambre no es legítima ni eficaz”

Tutaendelea kuvumilia mauaji ya aina hii yaendelee? Mahakama ilitoa maamuzi ya mwisho. Hakimu alitoa maamuzi ya mwisho na hivyo, nafikiri kuwa, kama walifanya makosa, kususia kula si sahihi kwa mujibu wa sheria na si njia muafaka.

Mgogoro

Video ifuatayo, iliyopakiwa na mtumiaji wa Youtube aitwaye PipeHenriquezO, amefupisha mgogoro huu wa Mapuche nchini Chile katika video inayochukua muda wa sekunde 30. Lengo la mgogoro huu ni kuhusu kutunza na kuwa na uhuru na ardhi waliyokuwa wanaitumia kwa karne nyingi na sasa zinatumiwa kama hifadhi zao za asili:

Pia, katika Lindi kuu la Hisia Kinzani blogu ya Tumblr, unaweza kupata hifadhi ya picha za historia ya harakati za Mapuche.
Watumiaji wa mtandao pia wametoa maoni yao mbalimbali kuhusiana na maandamano haya wakiiunga mkono jamii ya Mapuche, hatua zinazochukuliwa na serikali pamoja na taarifa tofauti tofauti zilizotokana na jambo hili. Maoni yanakinzana.

Alejandro Bascur, Mwanahabari na mchezaji wa mchezo wa Golfu, (@AlejandroBascur) [es] alikuwa na furaha mara baada ya kipindi cha televisheni kuoneshwa katika televisheni ya Taifa:

@AlejandroBascur: Notable informe especial TVN. Al fin se Muestra el terror q siembran los mapuches en el sur, sin ningún respeto por DDHH #InformeEspecial

@AlejandroBascur: Taarifa kubwa na maalumu iliyooneshwa na TVN ( Televisheni ya Taifa ya Chile). Hatimaye wanaonesha hali ya woga iliyopandikizwa upande wa Kusini na Mapuche, bila ya kujali haki za binadamu kabisa. #InformeEspecial

Akirejea matamko ya Rais Piñera, mwandishi wa habari na mwanablogu [es] Francisco Méndez (@Franmen) [es] anafafanua kuwa:

@Franmen: El Presidente Piñera podría prestar el mismo respaldo que brinda a policías ,a los estudiantes y a los Mapuche cuando se los estigmatiza

@Franmen: Rais Piñera angeweza kuwasaidia wanafunzi walioshutumiwa pamoja na Mapuche kama anavyowasaidia polisi

Zaidi, Pedro Cayuqueo ambaye ni mwanahabari wa Mapuche, mwandishi na mwanablogu Pedro Cayuqueo (@pcayuqueo) [es] alifafanua kwa kujiamini:

@pcayuqueo: Cuesta hablar del trasfondo del tema mapuche cuando lo que gatilla los debates es la cronica policial. Aun asi, algunos lo intentamos.

@pcayuqueo: n Ni vigumu kuongelea chimbuko la jambo hili la Mapuche wakati kinachochochea mijadala ni matukio ya muda mrefu ya polisi. Hata hivyo, baadhi yetu tunajaribu.

Wakati huo huo, mwanablogu Punngey aliweka mawazo [es] yafuatayo katikaTumblr kufuatia kusitishwa kwa mgomo wa kutokula:

HOY, 60 días de ayuno…se acabó el conteo, 60 días de sacrificio por que la verdad saliera a flote, 60 días de lucha de coraje, de orgullo, de ese orgullo que acompaña a cada uno de quienes SOMOS mapuche, aunque hayan algunos por ahí que digan que ya no existimos, esperemos que esta lucha acabe pronto […] a seguir luchando por que se vayan las forestales y represas de nuestras tierras, por la sanación de nuestra mapu, a seguir recuperando lo que se nos usurpó, y por fin caminar libres por nuestra mapu, que nuestros hijos no sigan creciendo con la represión en sus sueños…y que ellos si caminen por las tierras libres de nuestros abuelos…AMULEPE TAIÑ WEICHAN!!! WEWAIÑ. LA LUCHA CONTINÚA…

LEO, siku 60 za kufunga… hesabu imefikia tamati, siku sitini za kutjitoa sadaka ili kuujua ukweli, mapigano ya siku 60 yaliyo ya hamasa, ya kujivunia, pongezi zinazomhusu kila mmoja wetu aliye mtu wa Mapuche, pamoja na kuwa wapo wanaosema sisi hatupo tena. Tunategemea harakati hizi kuisha mapema iwezekanavyo. Tuendeleze juhudi zetu ili mashirika ya misitu na mabwawa wtuachie ardhi yetu, kwa kuitunza ardhi yetu, ili tuendelee kurejesha kila kilichochukuliwa kutoka kwetu na mwisho tutembee kwa uhuru kwenye (mapu) ardhi yetu ili watoto wetu wasiendelee kukua wakigubikwa na ndoto za ukandamizwaji…. na kuwa wataweza kutembea katika ardhi iliyo huru ya mababu zao….AMULEPE TAIÑ WEICHAN!!! WEWAIÑ. HARAKATI ZINAENDELEA….

Bendera ya Mapuche iliyowekwa na mtumiaji wa Flickr aitwaye Diego Martin (CC BY-NC-ND 2.0)

1 maoni

jiunge na Mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.