Venezuela: Picha za Siku ya Uchaguzi

Leo, mitandao ya kijamii nchini Venezuela imekuwa ikitoa taswira ya nchi hiyo kuwa ukingoni mwa zoezi muhimu. Pamoja na shuhuda mbalimbali, taarifa, tetesi na mapendekezo, majukwaa ya vyombo vya habari vya kijamii kama vile Twita, Facebook na Flickr yameonyesha picha zinazoonyesha ushiriki mkubwa wa raia katika kumchagua Rais ajaye wa Jamhuri hiyo.

Kwa mujibu wa maoni kadhaa, baadhi ya vituo vya upigaji kura vilifunguliwa usiku wa manane wa siku ya Jumamosi, ambapo wasimamizi wasaidizi wa zoezi hilo waliruhusiwa kuingia, na kuwapa fursa raia kutoka ndani na nje ya nchi kupiga kura.

Maritza Salazar (@MaritzaSalazar) [es] aliweka picha hii ya wapiga kura wakiwa katika foleni ndefu tangu usiku wa kuamkia uchaguzi:

Foto compartida por @maritzasalazar en Twitter

Picha na @maritzasalazar kupitia mtandao wa Twita

Fernando Rios (@FernandoRiosD) [es] aliweka picha ya Carlos Urbaneja, raia mwenye miaka 94 ambaye namba yake ya utambulisho ni 5 na ayekwenda kutumia haki yake ya kuchagua:

Foto compartida por @FernandoRiosD en Twitter

Picha imewekwa na @FernandoRiosD kupitia mtandao wa Twita

Kwa kupitia alama habari #NoEsUnaColaEsUnCamino [es] (si foleni, ni barabara) inayorejea kauli mbiu ya Henrique Capriles “kuna barabara”; watumiaji wa mtandao wa twita wametuma mtandaoni picha za vituo vya upigaji kura, foleni ndefu, ujumbe wa matumaini, na vidole vilivyochonywa wino usiofutika unaothibitisha pasi na shaka kwamba mhusika amepiga kura.

Carlos Garcia (@carlosgarciareq) [es] na Mirian de Aristimuño (@MiriamJSdeA) [es] walionyesha vidole vyao vilivyochonywa wino usiofutika kupitia alama habari #yavote [es] (Nimeshapiga kura yangu):

Foto compartida por @MiriamJSdeA en Twitter

Picha imewekwa na @MiriamJSdeA kupitia mtandao wa Twita

Foto compartida por @carlosgarciareq en Twitter

Picha imewekwa na @carlosgarciareq kupitia mtandao wa Twita

Vilevile, Martha Evelyn Batres (@Tita_Batres) [es] alipandisha picha zilizoonyesha idadi kubwa ya watu wakishiriki uchaguzi huo:

Foto compartida por @Tita_Batres en Twitter

Picha zimewekwa na @Tita_Batres kupitia mtandao wa Twita

Zaidi ya hayo, blogu ya The Devil's Excrement iliweka picha kadhaa zinazoonyesha foleni ndefu za watu jijini Caracas na hata nje ya Venezuela:

Liceo Andrés Bello, foto compartida por el blog The Devil's Excrement

Shule ya Andrés Bello, picha iliwekwa awali kwenye blogu ya The Devil's Excrement

Jessica Carrillo alishiriki katika uandaaji wa posti hii.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.