Oktoba, 2012

Habari kutoka Oktoba, 2012

China: Hatua za Kubana Uhuru wa Habari Majimboni

  15 Oktoba 2012

Jing Gao kutoka blogu ya Tofu anaeleza namna serikali ya Fuji ilivyo na mikakati michafu dhidi ya Yunnan na jinsi inavyochukua hatua za kuzuia uchapishaji wa habari zinazoweka wazi kashfa za ufisadi zinazomkabili afisa mmoja wa serikali.

Guatemala: Waandamanaji Wazawa 7 Wauawa Totonicapán

  13 Oktoba 2012

Raia wasiopungua 7 wameuawa, takribani watu 32 wamejeruhiwa na 35 walidhuriwa na sumu mnamo tarehe 4, Oktoba, 2012 wakati majeshi ya muungano yalipotumia nguvu kuwatawanya waandamanaji kutoka katika njia panda maarufu inayoeleka jiji la Guatemala City.

Venezuela: Ni Chávez Tena kwa Miaka Sita Zaidi

  11 Oktoba 2012

Baada ya chaguzi zilizokuwa na changamoto na ushindani mkubwa katika muongo uliopita, Venezuela itaongeza miaka mingine sita kwa utawala wa Hugo Chávez Frías ulioanza mwaka 1999. Idadi ya watu waliokuwa mtandaoni hasa kwenye mitandao ya kijamii, hasusani twita, ilikuwa kubwa sana hasa kabla matokeo rasmi hayajatangazwa.

Uganda Yaadhimisha Miaka 50 ya Uhuru

Terehe 9 Oktoba, 1962, Uganda ilijipatia uhuru wake kutoka kwa Mwingereza. Wakati nchi hiyo iliposherehekea Kumbukumbu yake ya Dhahabu hivi karibuni, wa-Ganda wanaotumia mtandao wamekuwa wakitumia zana za kijamii kama Twita na Facebook kusema maoni yao kuhusu sherehe hizo za kutimiza miaka 50!

Je, Una Swali Lolote kwa Jimmy Carter?

  10 Oktoba 2012

Rais wa zamani wa Marekani Jimmy Carter anapokea maswali kupitia mitandao ya kijamii ya Facebook na Twita (#CarterQA) kama sehemu ya kuadhimisha miaka 30 ya Kituo cha Carter (Carter Center) kinachojishughulisha na “kupigania masuala ya amani na kupambana na magonjwa duniani kote”. Rais Carter atakuwa anayajibu maswali hayo kwa njia...

Trinidad na Tobago: Ufisadi na Utawala wa Sheria

  9 Oktoba 2012

Hivi karibuni, masuala ya utawala wa sheria yamekuwa yamekuwa yakitawala serikali iliyoko madarakani. Kwa kuwa na kipengere cha 34 ambacho hakifahamiki sana miongoni mwa wananchi, hali ya mambo imebadilika na kuwa utawala wa kiimla, na […] tunaweza kuona ufisadi na matumizi mabaya ya madaraka yamebadilisha kabisa tabia za wale tuliowaona...

Tunisia: Mgomo Waanza jijini Thala

Kupitia mtandao wa twita, Tounsia Hourra (m-Tunisia huru) anasema [ar] kuna mgomo mkubwa umeanza jijini Thala, kwenye jimbo la Kasserine, leo [Oktoba 8, 2012]. Mgomo huo umekuja kama hatua ya kupinga kukua kwa kasi kwa ukosefu wa ajira na kuzorota kwa maendeleo ya jiji hilo. @tounisiahourra: اضراب عام في تالة...

Uarabuni: Sera ya Romney kwa Mashariki ya Kati Yaibua Mjadala

Hotuba ya Mgombea urais wa Marekani kupitia chama cha Republican Bw. Mitt Romney iliyoelezea sera yake ya nje imeibua mjadala mzito miongoni mwa raia wa mtandaoni leo hasa wale watokao katika nchi za ki-Arabuni. Twiti zinazohoji sera ya mambo ya nje ya Marekani kwa Mashariki ya Kati ziliendelea wakati ambao Romney, anayepeperusha bendera ya chama cha Republican, alipozungumza katika Chuo cha Jeshi cha Virginia. Endapo atachaguliwa, Romney ameahidi kuwa na sera rafiki za mambo ya nje, tofauti na mwelekeo usiotabirika wa sera za Obama wakati huu ambapo mabadiliko ya kisiasa yanaendelea kulikumba eneo la Mashariki ya Kati.

Venezuela: Picha za Siku ya Uchaguzi

  8 Oktoba 2012

Leo, mitandao ya kijamii nchini Venezuela inatoa taswira ya nchi hiyo kuwa ukingoni mwa zoezi muhimu. Pamoja na shuhuda mbalimbali, taarifa, tetesi na mapendekezo, majukwaa ya vyombo vya habari vya kijamii kama vile Twita, Facebook na Flickr yameonyesha picha zinazoonyesha ushiriki mkubwa wa watu katika kumchagua Rais ajaye wa Jamuhuri hiyo.