- Global Voices in Swahili - https://sw.globalvoices.org -

Misri: Ushauri kwa Waandamanaji wa Kuwait

Mada za Habari: Mashariki ya Kati na Afrika Kaskazini, Kuwait, Misri, Maandamano, Siasa, Uandishi wa Habari za Kiraia, Vichekesho

Wakati watu wa Kuwait walipoanzisha maandamano makubwa ambayo hayakuwahi kutokea [1] ya kuonesha waziwazi kutokukubaliana na mabadiliko ya sheria ya uchaguzi yaliyopitishwa chini ya mtawala wa kurithi kufuatia kuvunjwa kwa bunge, watu wa Misri wametumia muda wao mwingi katika Twita wakitoa ushauri kwa watu wa Kuwait kuhusiana na yapi ya kufanya na yapi ya kutokufanya.

Samah Anwar amejikita katika kujadili namna ya uvaaji ya wanaume wa Kuwait, ambao wanavaa namna fulani ya kanzu iitwayo thobe. Anatwiti kuwa [ar]:

لبس الجلبيات ده مينفعش خالص ف الثورات

@samahanwar [2]: Kuvaa kanzu aina ya thobe si vazi muafaka katika harakati za mapinduzi

Katika ujumbe mwingine wa Twita, Samah Anwar anatoa sababu:

ماتجبوش الخراب لبلدكم انتو عايشين كويس واحمدو ربنا غيركم مش لاقي العيش

@samahanwar [3]: Usiiangamize nchi yako. Unaishi vizuri. Mshukuru Mungu kwa kila unalojaaliwa. Watu wengine wanashindwa kuishi.

Watu wengi wa Misri walikuwa na mawazo yanayofanana. Ebrahim Elkhadm anaandika[ar]:

#نصيحة_مصرية_للكوايته.. تبقوا ولاد مره لو سمعتوا كلامنا .. ده احنا اساسا معرفناش ننصح نفسنا بلا هبل

@ebrahimelkhadm [4]: Mtapotea kama mkitusikiliza sisi. Sisi wala hatujui namna ya kujishauri.

Elshazli anaongeza:

ركزوا فى كل كلمة مكتوبة فى الهاشتاج دا واعملوا عكسها هتلاقوا ثورتكم نجحت

@El_Shazli [5]: Zingatia kila neno linaloandikwa katika kiungo habari hiki na kisha ufanye kinyume chake. Utagundua kuwa mapinduzi yako yamekuwa ya mafanikio.

Egyptians advise protesting Kuwaitis on Twitter [6]

Watu wa Misri wawashauri waandamanaji wa Kuwait katika Twita. Naser AlMufarrij kutoka Kuwait aweka picha hii katika Twita


And Kuwaiti Naser AlMufarrij aweka [6] Picha hii kutoka Twita iliyo katika lugha ya Kiarabu:

Kwanini mnafanya mapinduzi wakati mtoto mdogo kabisa miongoni mwenu ni tajiri kuliko waziri wa Misri?

Watu wengi wa Misri walitumia mwanya huu kukejeli mapinduzi yao wenyewe, kama Gepril Thuwaiba anavyotwiti:

قبل ما تتحركوا المره اللى جايه كل واحد يتفق مع صحابه ..بعد المسيره مفيش كلام ولا جدال والا الفراق

@Gepril1 [7]: Wakati mwingine kabla ya kuingia mitaani, kila mmoja lazima akubaliane na marafiki zake. Baada ya matembezi ya maandamano, usiongee, hoji na kila mtu atawanyike.

Anaongeza kuwa:

هما ثلاث خطابات لو حصل مبروك عليكوا متنسوناش بعد الفرحه الكبيره كام برميل كده ع الماشى احسن الحاله ضنك

@Gepril1 [8]: Kuna hotuba tatu tu [kwa kurejea hotuba tatu za Mubarak kabla ya kutoka madarakani]. Kama hilo linatokea, ninawapongeza! Baada ya kusherehekea sana, msitusahau. Tukumbukeni kwa mapipa kadhaa tu ya mafuta kwa kuwa hali yetu huku si nzuri.

Watu wa Kuwait waliweka bayana kuwa maandamano ya Kuwait yalikuwa ni “maandamano tu” na siyo mapinduzi. Barcelonya anafafanua:

دي مش ثورة دا احتجاج يا اخوانا

@Barcelonya [9]: Haya si mapinduzi, ni maandamano.

Lakini Mona Abo Elyazeed anaendelea kushikilia msimamo kutokana na ushauri alioutoa na anaweka maoni yake:

@MonaAbo [10]: Hakuna maridhiano