- Global Voices in Swahili - https://sw.globalvoices.org -

Madagascar: Global Voices katika Kimalagasi Yapiga Hatua Kubwa

Mada za Habari: Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara, Madagaska, Harakati za Mtandaoni, Lugha, Uandishi wa Habari za Kiraia, Vijana, Matangazo, Wasifu wa Wanablogu
[1]

Mradi wa Lingua wa Global Voices katika lugha ya Ki-Malagasi

Mradi wa Lingua wa Global Voices katika lugha ya ki-Malagasi [1] umechapisha mtandaoni posti yake ya 5,000 [2]. Mradi huo ulianza mwezi Septemba 12, 2007 [3] ukiwa kati ya miradi ya mwanzo kabisa ya  Mradi mkubwa wa Lugha za Kiafrika [4]. Kwa sasa mradi huo unaendeshwa na watafsiri wa ki-Malagasi [5] wapatao 16 miongoni mwao akiwamo mmoja wa watafsiri wadogo kabisa wa Global Voices [6], mwenye umri wa miaka 16 aitwaye Radifera Felana Candy [7].