- Global Voices in Swahili - https://sw.globalvoices.org -

Je, Una Swali Lolote kwa Jimmy Carter?

Mada za Habari: Marekani ya Kaskazini, Marekani, Afya, Mawazo, Mwitikio wa Kihisani, Uandishi wa Habari za Kiraia

Rais wa zamani wa Marekani Jimmy Carter anapokea maswali [1] kupitia mitandao ya kijamii ya Facebook [2] na Twita [3] (#CarterQA [4]) kama sehemu ya kuadhimisha miaka 30 ya Kituo cha Carter (Carter Center) kinachojishughulisha na “kupigania masuala ya amani na kupambana na magonjwa duniani kote”. Rais Carter atakuwa anayajibu maswali hayo kwa njia ya video tarehe 19 Oktoba, 2012.