- Global Voices in Swahili - https://sw.globalvoices.org -

Ghana: Vikwazo Vinavyowakabili Wanawake Kimaendeleo

Mada za Habari: Ghana, Habari za Wafanyakazi, Siasa, Uandishi wa Habari za Kiraia, Utawala, Wanawake na Jinsia

Betty Mould Iddrisu [1], Jaji na Waziri wa Sheria wa Ghana, anaandika [2] [fr] kwenye blogu ya pambazuka.org:

Kufikia ngazi za juu kabisa za utawala si rahisi, na hata unapopanda mpaka juu kabisa, bado unajikuta unakabiliwa na hisia za watu zenye uadui na watu wanakuwa na mashaka na uwezo wako, kwa sababu tu wewe ni mwanamke. Mwanamke akikamata madaraka ya juu humbidi kufanya kazi kwa bidii zidi kuliko mwanaume ili kuthibitisha uwezo wake, lakini bado hata akifanya hivyo anakumbana na uadui pamoja na mfumo unaomwona kuwa duni, iwe katika majukumu yake kama meneja na kiongozi, na hata katika mazingira yoyote ya kazi ambayo yanatawaliwa kwa kiasi kikubwa na wanaume.