- Global Voices in Swahili - https://sw.globalvoices.org -

Côte d'Ivoire: Wafanyakazi wa Afya Wagoma baada Miezi Minne Bila Mshahara

Mada za Habari: Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara, Cote d'Ivoire, Afya, Habari za Wafanyakazi, Sheria, Uandishi wa Habari za Kiraia, Uchumi na Biashara, Utawala

S.B anatoa maoni juu ya kuanza kwa mgomo usio na ukomo unaoratibiwa na wafanyakazi wa taasisi za afya mjini Abidjan. Katika mtandao wa Connection Ivorienne, anabainisha [1] [fr] kwamba:

Kufuatia mabadiliko ya utolewaji wa huduma za afya ambazo zilitolewa bure kabisa baada tu ya kumalizika kwa mgogoro wa baada ya uchaguzi, sera iliyoanzishwa na serikali ya Côte d'Ivoire, ambayo sasa imeelekeza baadhi ya huduma tu ndizo zitakuwa bure, wafanyakazi wa taasisi kadhaa za afya hawajapata mishahara yao kwa wakati. Kibaya zaidi ni kwamba wakubwa wao hawakupata fungu lolote kwa ajili hiyo kwa zaidi ya miezi kumi na sita.