8 Oktoba 2012

Habari kutoka 8 Oktoba 2012

Tunisia: Mgomo Waanza jijini Thala

Kupitia mtandao wa twita, Tounsia Hourra (m-Tunisia huru) anasema [ar] kuna mgomo mkubwa umeanza jijini Thala, kwenye jimbo la Kasserine, leo [Oktoba 8, 2012]. Mgomo huo umekuja kama hatua ya kupinga kukua kwa kasi kwa ukosefu wa ajira na kuzorota kwa maendeleo ya jiji hilo. @tounisiahourra: اضراب عام في تالة...

Uarabuni: Sera ya Romney kwa Mashariki ya Kati Yaibua Mjadala

Hotuba ya Mgombea urais wa Marekani kupitia chama cha Republican Bw. Mitt Romney iliyoelezea sera yake ya nje imeibua mjadala mzito miongoni mwa raia wa mtandaoni leo hasa wale watokao katika nchi za ki-Arabuni. Twiti zinazohoji sera ya mambo ya nje ya Marekani kwa Mashariki ya Kati ziliendelea wakati ambao Romney, anayepeperusha bendera ya chama cha Republican, alipozungumza katika Chuo cha Jeshi cha Virginia. Endapo atachaguliwa, Romney ameahidi kuwa na sera rafiki za mambo ya nje, tofauti na mwelekeo usiotabirika wa sera za Obama wakati huu ambapo mabadiliko ya kisiasa yanaendelea kulikumba eneo la Mashariki ya Kati.

Venezuela: Picha za Siku ya Uchaguzi

  8 Oktoba 2012

Leo, mitandao ya kijamii nchini Venezuela inatoa taswira ya nchi hiyo kuwa ukingoni mwa zoezi muhimu. Pamoja na shuhuda mbalimbali, taarifa, tetesi na mapendekezo, majukwaa ya vyombo vya habari vya kijamii kama vile Twita, Facebook na Flickr yameonyesha picha zinazoonyesha ushiriki mkubwa wa watu katika kumchagua Rais ajaye wa Jamuhuri hiyo.

Venezuela: ‘Sura na Sauti’ za Uchaguzi

  8 Oktoba 2012

Kwa kutumia mfululizo wa picha na nukuu, mpiga picha wa Kireno Eduardo Leal anayateka mawazo na hisia za watu wa Venezuela kwa jinsi zinavyoeleza watakuwa wanampigia nani kura kuwa Rais katika uchaguzi uliofanyika Jumapili ya Oktoba 7.Kwa kutumia mfululizo wa picha na nukuu, mpiga picha wa Kireno Eduardo Leal anayateka mawazo na hisia za watu wa Venezuela kwa jinsi zinavyoeleza watakuwa wanampigia nani kura kuwa Rais katika uchaguzi uliofanyika Jumapili ya Oktoba 7.