Palestina: Maandamano Yalipuka Kupinga Ongezeko la Bei za Bidhaa na Ukosefu wa Ajira

Maandamano yanazidi kushamiri katika nchi ya Palestina hususani katika majiji ya Ukanda wa Magharibi ambayo ni: Hebron, Ramallah, Bethlehem na Nablus. Waandamanaji wanaonesha hasira yao kwa mamlaka ya Palestina wakilalamikia gharama kubwa za maisha pamoja na ongezeko kubwa la vijana wa Palestina wasio na ajira.

Maandamano yalianza mara baada ya mamlaka ya Palestina kutangaza kuongeza bei za mafuta na petroli kwa takribani asilimia 8 katika ukanda wa Magharibi, bei zitakazaoanza kutumika mwazoni mwa mwezi Septemba. Kwa hiyo, ongezeko hili lilisababisha kuongezeka kwa bei za bidhaa, bila ya kuongezeka kwa mishahara wala ujira katika nchi ya Palestina.

Aban Idrees alishuhudia maandamano jijini Hebron na alitwiti[ar]:

@abanidrees: في مدينة الخليل شلل تام في حركةالمرور بعد إحتجاجات اليوم ضد الغلاء والمطالبة بإسقاط حكومة فياض حيث لا تكاد سيارة تتحرك في الشارع
Jijini Hebron, magari yamezuiwa kuendelea na safari kabisa baada ya maandamano ya kupinga mfumuko wa bei za bidhaa wakishinikiza serekali ya Fayyad kujiuzulu. Ni magari machache sana yanaonekana kupita katika mitaa

Mwanablogu Ola Al Tamimi pia alitwiti kutokea Hebron [ar]:

@OlaAlTamimi: شارع عين سارة أكبر شوارع الخليل مغلق بالشاحنات وأجساد الناس .. وبدأت بعض الناس بالتحرك باتجاه مقر الأمن الوطني ومبنى المحافظة
Ain Sarah, mtaa mkubwa wa Hebron, kwa sasa umejaa magari na watu. Maandamano mengine yanaanza kuelekea makao makuu ya usalama wa taifa pamoja na jengo la baraza la mji (Manispaa)

Ola aliongeza[ar]:

@OlaAlTamimi:أول مرة بتاريخ الخليل بتصير مظاهرة وما في حدا بنضرب من أجهزة الأمن الوقائي
Hii ni mara ya kwanza kwa maandamano kutokea Hebron bila ya mtu yeyote kushambuliwa na askari wa kuzuia ghasia.

Hafez Omar, Mpalestina mwanaharakati na msanii alitwiti[ar]:

@hafezomar:لأول مرة منذ العام ١٩٣٦ يتظاهر الفلسطينيون من أجل لقمة العيش!! العار لمن يريدنا أن ننسى فلسطين جريا وراء رغيف الخبز…
Hii ni mara ya kwanza tokea mwaka 1936 tangu Wapalestina walipoandamana kwa ajili ya kulalamikia kupanda kwa gharama za maisha. Ni aibu kwa yeyote anayetutaka tuisahau Palestina na tukimbilie kupigania mkate….

Mtandao wa Twita pia ulifurika misemo mingi ya utani iliyowekwa na waandamanaji wa Palestina. Rana Baker alitwiti [ar]:

@RanaGaza: من أجمل الشعارات التي رفعت اليوم في فلسطين ضد حكومة ‎‫فياض‬‏ و غلاء الأسعار: “صرت أنزل ع السوق أعمل Like و أروح.” ‎‫‬‏
Miongoni mwa mabango bora yaliyokuwa yameinuliwa leo na wa-Palestina linaloipinga serikali ya Fayyad na ongezeko la gharama lilisomeka: “Siku hizi ninapoenda sokoni, ninabofya tu kitufe cha ‘kupenda’ na kisha ninarudi zangu nyumbani!”

Bango jingine lilinaswa na mpiga picha Lamees Suradi:

@lames7: The nicest comment from Nablus: “If you are not standing with the poor then you are not standing with the prisoners either; please explain to us why are you still in power!”

@lames7: Maoni mazuri zaidi kutoka kwa Nablus: “kama huwezi kuwatetea masikini, basi haupo kuwatetea wafungwa vile vile; tafadhali tuambie ni kwa nini bado uko madarakani!”

Mtumiaji wa Twita, iPalestine alitwiti kuhusiana na jaribio la kutaka kujitoa mhanga kwa mtu aliyejulikana kwa jina la Hussein Qahwaji [ar]:

@PFLP67: مواطن قام بسكب البنزين على جسده وجسد ابنته البالغة من العمر 5 سنوات وحاول إحراق نفسه لكن المواطنين منعوه بالقوة.
Mkazi mmoja wa ukanda wa Gaza, Hussein Qahwaji, alijimwagia mafuta ya taa mwili mzima kwa lengo la kujichoma lakini watu wengine walimzuia kwa nguvu ili asifanye hivyo.

Baadhi ya taarifa zinasema kuwa mtoto wa kike wa Qahwaji anasumbuliwa na saratani na anapata matibabu huko Jordani na kwamba Qahwaji hakuweza kumtembelea na ailiamua kujiunguza kwa moto ili kuishinikiza mamlaka ya Palestina imsaidie fedha ili akamjulie hali mtoto wake.

Haikuwa mara ya kwanza kwa M-palestina kutumia njia ya kujitoa mhanga kwa kujichoma kama njia ya kuonesha kutoridhishwa na jambo. Septemba 2, huko Gaza, mtu mwenye umri wa miaka 17, Ehab Abu al-Nada alikufa baada ya kujiunguza kwa moto, labda akifuata nyayo za m-Tunisia Mohamed Bouazizi. Ehab Abu al-Nada aliacha kuendelea na masomo na badala yake alikuwa akifanya kazi kwa takribani masaa 13 kila siku ili kujipatia ujira wa shekel 13 tu (karibu sawa na dola za kimarekani 7.4) ili aweze kumsaidia baba yake kuihudumia familia yao.
Jambo hili liliwagusa wengi, haswa mara baada ya picha ya kiongozi wa Hamas Ismail Haniyeh akiwa na baba yake Ihab, kuwekwa mtandaoni; Hanyeh alimtembelea ili ‘kumpatia msaada wa dharura’ wa dola za Marekani 2,000 kufuatia kifo cha Ehab.
Wengi wanafikiri kama harakati hizi zitaendelea, na kama zitaweza kuenezwa katika miji na majiji mengine. John Loyndon aliuliza:

@johnlyndon1: Kujitoa mhanga kwa kujiunguza kwa moto katika mji wa Gaza; kujichoma kwa moto kwa Fayyad huko Hebron; maandamano katika majiji muhimu huko ukanda wa Magharibi. Je, maandamano ya kuipinga serikali yanakuja Palestina kwa kuchelewa?

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.