Habari kutoka 19 Septemba 2012
Je, Sifa ya ‘Kisiwa cha Amani’ Tanzania Imeanza Kutoweka?
Tanzania imeshuhudia matukio kadhaa mabaya tangu kufanyika kwa uchaguzi mkuu wa 2010. Tukio la hivi karibuni ni kifo cha kikatili cha mwandishi wa habari wa Tanzania Daudi Mwangosi, aliyeuawa kwa bomu la machozi huko Iringa, Kusini mwa Tanzania, wakati polisi walipojaribu kukitawanya kikundi cha wafuasi wa chama cha upinzani.
Kocha Mfaransa Ateuliwa Kuongeza Bahati ya Kenya Kwenye Kandanda
Shirikisho la Kandanda nchini Kenya FKF, limemchagua Kocha mpya wa timu ya taifa la Kenya ambaye ni Mfaransa, Henri Mchel. Wanakamati hao, wana matumaini kuwa anaweza kuwa 'bahati' ya Kenya katika mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika ya 2013 na Kombe la Dunia la 2014.