- Global Voices in Swahili - https://sw.globalvoices.org -

Brazil: Mtoto wa Miaka 13 Aonyesha Matatizo ya Shule Kupitia Facebook

Mada za Habari: Amerika Kusini, Brazil, Elimu, Harakati za Mtandaoni, Mawazo, Uandishi wa Habari za Kiraia, Vijana

Diário de Classe [1] [pt], ukurasa wa Facebook uliofunguliwa na Isadora Faber, aliye na miaka 13 na anayetokea Santa Catarina, Brazil, tayari umeonyesha kupendwa zaidi ya mara 176,000. Huku lengo lake likiwa ni “kuonyesha ukweli kuhusu shule za umma”, Isadora anaweka picha zinazoonyesha maeneo yanayohitaji kufanyiwa ukarabati katika shule yake pamoja na kutoa taarifa kuhusu matatizo mengine mengi ya jumla.